Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Mzozo wa kisiasa nchini Somalia kati ya rais na Waziri Mkuu
Wiki hii rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, anayefahamika kwa jina lingine la Farmajo, alitangaza kumsimamisha kazi Waziri Mkuu Hussein Roble, kwa madai ya ufisadi kuhusu kashfa ya unyakuzi wa ardhi.Hata hivyo, Roble ameelezea hatua ya rais Farmajo kama jaribio la mapinduzi na kuapa kuendelea na majukumu yake.29/12/202109:33 -
Wakaazi wa GOMA mkoani Kivu kaskazini wapinga utovu wa usalama mashariki ya DRC
Makala ya wimbi la siasa inaangazia maandamano ya mamia ya waakazi wa mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakipinga utovu wa usalama na ripoti kuwa, serikali nchini humo imeingia kwenye makubaliano na nchi jirani ya Rwanda, kutuma polisi wake, kulinda usalama mjini Goma. Katika siku za hivi karibuni hasa mjini Goma katika mkoa wa Kivu Kaskazini, kumeshuhudiwa visa vya watu kuvamiwa, kutekwa nyara na kuuawa akiwemo mwanaharakati wa Lucha.Wakati wa maandamano hayo wiki hii, kuliropitiwa kuuawa kwa watu wanne, akiwemo afisa wa polisi na mtoto, baada ya kutokea kwa makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama. Kuelewa nini chanzo cha utovu wa usalama katika eneo hilo, ungana na mwandishi wetu Victor Abuso22/12/202110:09 -
Jeshi la Uganda litawamaliza waasi wa ADF nchini DRC ?
Jeshi la Uganda, limeanza mashambulizi dhidi ya waasi wa ADF Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kupata idhini kutoka kwa serikali ya Kinshasa. Je, hatua hii itasaidia kulimaliza kundi hili ambalo limesababisha maelfu ya raia ?01/12/202109:53 -
Hali ya kisiasa nchini Sudan baada ya Abdalla Hamdock kurudishiwa madaraka
Wiki hii kwenye tunaangazia hatua ya Jeshi nchini Sudan, kumrejeshea madaraka Waziri Mkuu Abdalla Hamdock baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi mmoja uliopita. Pande zote zilitia saini mkataba wa kisiasa. Tunajadiliana.24/11/202109:56 -
Hali ya kisiasa nchini Sudan baada ya jeshi kuipindua serikali ya kiraia
Nchini Sudan, jeshi limefanya mapinduzi na kuchukua serikali kutoka kwa kiongozi wa kiraia, Waziri Mkuu Abdalla Hamdok. Nini hatima ya Sudan ? Tunachambua.27/10/202110:01 -
Siasa za Tume ya Uchaguzi nchini DRC kuelekea Uchaguzi 2023
Wanasiasa wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka muungano wa Lamuka na Ensamble wamekataa uteuzi wa Dennis Kadima kuwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Uchaguzi CENI kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2023. Itakuwaje ? Tunachambua.20/10/202109:22 -
Sera za wanasiasa wanaotafuta urais nchini Kenya
Nchini Kenya, wanasiasa wanaendelea kunadi sera zao, kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2022. Miongoni mwa wanasiasa hao ni Raila Odinga na William Ruto. Tunachambua.13/10/202110:17 -
Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania kuelekea Uchaguzi 2025
Wiki hii tunaangazia hatua ya vyama vya siasa nchini Tanzania kuunda Baraza la pamoja kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.02/09/202109:32 -
Mvutano wa kumpata Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC
Viongozi wa dini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia wameshindwa kuelewana kuhusu ni nani awe Mwenyekiti mpya wa Tume ya Uchaguzi nchini humo CENI kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2023. Tunajadili19/08/202110:22 -
Nani atapeperusha bendera ya upinzani kwenye Uchaguzi Mkuu nchini Kenya ?
Wimbi la siasa wiki hii, linatupitia jicho siasa za upinzani, kumtafuta mgombea mmoja wa urais kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti mwaka 2022.13/08/202110:07 -
Kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani nchini Tanzania
Wiki hii, kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe alikamatwa na polisi akiwa mjini Mwanza, akijiandaa kuongoza kongamano la kudai katiba mpya nchini humo. Polisi wanasema wanamshikilia kwa tuhma za kigaidi.24/07/202109:18 -
Mvutano wa wanasiasa nchini Tanzania kudai Katiba mpya
Nchini Tanzania, wanasiasa wanaendelea kuzua mjadala kuhusu kuwepo kwa mchakato wa kupata katiba mpya, wakati huu rais wa nchi hiyo rais Samia Suluhu Hassan akisema hicho sio kipaumbele chake kwa sasa.09/07/202110:07 -
Shinikizo za Katiba mpya nchini Tanzania
Wanasiasa wa upinzani na wanaharakati nchini Tanzania wanaendelea kushinikiza upatikanaji wa Katiba mpya nchini humo. Tunachambua hili kwa kina.18/06/202110:19 -
Nini maana ya wanawake kuteuliwa kwa ngazi za juu serikalini Uganda?
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amewateuwa wanawake katika nyadhifa za juu serikalini, Nabbanja Nabbanja, akiteuliwa kuwa waziri mkuu,mwanajeshi mustaafu Jessica Alupo, akiteuliwa kuhudumu kama makamo rais.Victor Robert Wile, amezungumza na mchambuzi wa siasa za Uganda, Aida Mutenyo, kuelewa uteuzi huu.10/06/202109:07 -
Tanzani: Mvutano wa wabunge 19 wa viti maalum kutoka CHADEMA kuendelea kuwa bungeni
Chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA, kinaendelea kusisitiza kuwa hakikuidhinisha wabunge 19 wa viti maalum kutoka chama chake kwenda bungeni na kinataka waondolewe bungeni.08/05/202109:53
Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa