Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Tanzania: Tundu Lissu atangaza kurejea nyumbani
Mwanasiasa wa Tanzania, Tundu Lissu, baada ya kuishi uhamishoni kwa karibu miaka saba, ametangaza kuwa anarejea nyumbani Januari 25 2023, kuendeleza harakati za kisiasa, baada ya rais Samia Suluhu Hassan, kutangaza kuondoa marufuku ya vyama vya siasa, kufanya mikutano ya kisiasa.18/01/202310:04 -
M23 bado inashikilia baadhi ya maeneo mashiriki mwa DRC
Licha ya tetesi za kundi la M23 kudai kuchilia baadhi ya maeneo mashariki mwa DRC, taarifa sinasema waasi hao bado wanashikilia maeneo mengi mashariki mwa DRC.Skiza makala haya ufahamu mengi.16/01/202310:00 -
Kufutwa kwa kesi zinazowahusu wandani wa rais William Ruto
Tangu mwaka jana ,idara ya mahakama nchini Kenya imefuta baadhi ya kesi dhidi ya watu walio karibu na rais William Ruto05/01/202310:05 -
Siku mia moja za rais wa Kenya William Ruto ofisini na ahadi alizoahidi kutimiza ndani ya siku hizo
Disemba 22, rais wa Kenya William Ruto alitamatisha siku 100 ofisini, huku baadhi ya watu wakihoji kuhusu ahadi alizotoa kwa wakenya wakati wa kipindi cha kampeni na hata siku ya kuapishwa kwake.Moja ya aahdi alizotoa inayomgusa mwananchi wa kawaida moja kwa moja, ni kupunguza gharama ya maisha kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula.30/12/202210:00 -
Matukio ya kisiasa tuliyoyapa uzito mwaka 2022
Nchi mbalimbali, zikiongozwa na Ufaransa pamoja na Kenya, ziliandaa uchaguzi wake mwaka huu. Tulijadili matukio hayo kwa kina, na leo tunakukumbusha baadhi ya matukio hayo, japo kwa kifupi.21/12/202210:14 -
Mazungumzo ya amani kuhusu Mashariki mwa DRC yanafanyika jijini Nairobi
Makundi ya waasi, serikali ya DRC, mashirika ya kiraia na wadau wengine, wapo jijini Nairobi kwa ajili ya mazungumzo ya tatu ya amani, ili kuleta amani Mashariki mwa nchi hiyo. Je, suluhu itapatikana ?30/11/202209:47 -
Mkataba wa kuanzishwa mfuko wa fedha kushughulikia athari za mabadiliko ya tabianchi COP27
Katika mkutano wa kimataifa wa mazingira COP27, nchini Misri, mataifa karibu mia mbili yaliafikia makubaliano ya kuanzishwa kwa mfuko wa fedha wa kushughulikia hasara na uharibifu, fedha hizi zikitarajiwa kuzisaidia nchi masikini na zilizo katika hatari ya kuathirika zaidi na athari za mabadiliko ya tabianchi.25/11/202210:01 -
Juhudi za kidiplomasia kusaka amani Mashariki mwa DRC
Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, anaongoza jitihada za kidiplomasia kusaidia kuleta amani Mashariki mwa DRC, kuelekea awamu nyingine ya mazungumzo ya amani jijini Nairobi. Juhudi hizi zinaendelea wakati huu waasi wa M 23 yakiendelea kati ya jeshi la serikali, FARDC. Je, suluhu itapatikana ?16/11/202209:07 -
Mapigano mashariki mwa DRC.
Makala hii imeangazia hali ya usalama inayojiri huko mashariki ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, ambako Kundi la waasi wa M23 likiungwa mkono na Rwanda lilifanikiwa kuyateka miji miwili muhimu ya Rutshuru na Kiwanja mashariki ya DRC na kuendelea na mapigano kwenye viunga vya mliji hiyo, huku serikali ya Kinshasa ikichukua uamuzi wa kumfurusha Balozi wa Rwanda nchini humo, Vincent Karega huku Juhudi za kimataifa zikiendelea kuzipatanisha nchi hizo mbili.Kuangazia hili tumewaalika profesa Pacifique Malonga, ni mtaalamu wa sias aza Rwanda akiwa jijini Kigali nchini Rwanda naye Guerschom Kahebe ni mchambuzi na mtaalamu wa siasa za DRC akiwa Calfornia nchini Marekani.02/11/202209:58 -
Ongezeko la mapinduzi ya kijeshi Barani Afrika
Msikilizaji utaskia mengi kuhusu chanzo cha ongezeko la mapinduzi ya kijeshi barani Afrika.Mapinduzi kama haya yameshafanyika kwenye nchi za Guinea na Mali, huku majaribio mengine kadhaa yakishindikana kwenye ukanda huo.Mwaka 2021 ulishuhudia idadi kubwa ya mapinduzu barani Afrika ukilinganisha na miaka iliyopita.Leo tunaangazia kwa kina yanayotokea na pengine kutafuta suluhu26/10/202210:01 -
Mjadala kuhusu utovu wa usalama Mashariki mwa DRC
Mapigano yaendelea kushuhudiwa nchini DRC, kati ya jeshi la serikali FARDC na waasi wa M23, serikali ya Kinshasa ikiendelea kushtumu nchi jirani ya Rwanda kuwaunga mkono waasi. Juhudi za mazungumzo hadi sasa hazijafua dafu.26/10/202210:00 -
10:02
-
Mjadala kuhusu kuondolewa kwa mipaka ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Karibu katika Makala yetu leo wimbi la siasa, kwenye usukani uko nami Ali Bilali ambapo tunajadili kuhusu maendeleo ya jumuiya ya Afrika Mashariki hususan kuhusu kauli ya hivi karibuni ya rais mpya wa Kenya William Ruto, ambae amemuomba Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akiwa kama mkongwe miongoni mwa Viongozi wa Afrika Mashariki kupambana ili kuhakikisha mipaka inayotenganisha Nchi inaondolewa na kuondoa vikwazo vingine vyote.12/10/202209:56 -
Rais Macron anaweza kuwapatanisha, Kagame na Tshisekedi
Pembezoni mwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikutana na wenzake wa Rwanda, Paul Kagame na Felix Tshisekedi, kuona uwezekano wa wawili hao kufikia mkataba wa amani kuhusu utovu wa usalama, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.28/09/202210:09 -
Antonio Guterres : M23 ni tishio kwa MONUSCO
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amedai kwamba waasi wa M23 wana silaha nzito kushinda wanajeshi wa Umoja wa mataifa wanaohudumu nchini DRC, MONUSCO, akisema sharti mbinu tofauti itumike kuwashinda waasi hao .Katika makala haya tunathimini kauli hii ya Guterres.21/09/202209:49
Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa