Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Kukutana kwa kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga na rais Ruto kwenye hafla ya hadhara
Hii ni baada ya rais Ruto na Odinga mwishoni mwa wiki iliyopita, kuonekana hadharani pamoja, mwanzo katika mazishi ya mke wa mpiganiaji uhuru Dedan kimathi, Mukami Kimathi na baadaye katika mashindano ya riadha na mchezo wa soka Jumapili iliyopita.17/05/202309:59 -
SADC kutuma kikosi nchini DRC, Tshisekedi akosoa kikosi cha EAC
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amelishtumu jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutofanya vya kutosha kudhibiti utovu wa usalama Mashariki mwa nchi yake.Mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC, wamesema watatuma kikosi chake Mashariki mwa DRC, huku Umoja wa Mataifa ukita juhudi zaidi kusaidia kupatikana kwa amani. Tunachambua kwa kina.10/05/202310:17 -
Je serikali ya Kenya ianze kudhibiti makanisa
Karibu katika makala wimbi la siasa. Tunaangazia swala la mhubiria Paul Mackenzie Nthenge ambaye aliwashawishi wafuasi wa kanisa lake wafunge bila kula ili wakutane na Mungu katika kijiji cha Shakahola karibu na mji wa Malindi, Pwani ya Kenya.27/04/202309:59 -
Sudan: Majenerali waendelea kupimana nguvu licha ya juhudi za kidiplomasia
Wiki hii kwenye Makala wimbi la siasa, Jupiter Mayaka anafanya mwendelezo wa mzozo unaoendelea nchini Sudan, wakati huu hali ya kibinadamu ikizidi kuwa mbaya, kutokana na raia kuuawa na misaada kutowafikia waathiriwa.19/04/202310:00 -
Kucheleweshwa kwa kusainiwa kwa mkataba wa kisiasa nchini Sudan
Kwenye Wimbi la Siasa wiki hii, Ali Bilali anaangazia kucheleweshwa kwa kusainiwa kwa mkataba wa kisiasa nchini Sudan, utakaoruhusu kuundwa kwa serikali ya kiraia baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 2021.12/04/202309:48 -
Mchakato wa maridhiano kati ya serikali na upinzani nchini Kenya baada ya maandamano
Rais William Ruto na kinara wa upinzani Raila Odinga watoa nafasi ya kuzungumza kumaliza mzozo wa kisiasa06/04/202310:06 -
Je, suluhu ya kisiasa itazaa matunda kuhusu mzozo wa DRC
Suluhu ya kudumu kuhusu mzozo wa usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, haijapatikana mpaka sasa. Waasi wa M 23, wameendelea kupambana na wanajeshi wa serikali. Jumuiya ya Kimataifa, inasema suluhu ni ya kisiasa. Je, itawezekana ?Tunajadili hili na wachambuzi, Price Mugasalusha na Edwin Kegolu, kutoka kwenye ukumbi wa Alliance Francais jijini Nairobi.29/03/202310:01 -
Nini hatima ya mvutano wa kisiasa nchini Kenya ?
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ameitisha maandamano kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha na kuipinga serikali ya rais William Ruto kwa kile anachosema hakushinda uchaguzi wa urais wa mwaka uliopita. Nini suluhu ?24/03/202310:15 -
Nafasi ya wanawake kwenye siasa za bara Afrika
Leo tunatupia jicho nafasi ya wanawake kwenye siasa za bara Afrika. Wiki hii siku ya Jumapili tarehe 19 rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, anatimiza miaka mitatu madarakani, baada ya kuapishwa kuongoza nchi hiyo kama rais wa sita, na kuwa rais wa kwanza mwanamke.15/03/202309:55 -
Siku ya kimataifa ya wanawake duniani
Kauli mbiu ya sherehe za mwaka huu wa 2023 imekuwa ni matumizi ya kidigitali kwa usawa wa kijinsia na namna wanawake wanaweza kutumia teknolojia kuaangazia na kutafuta suluhu ya changamoto zao.10/03/202311:24 -
Harakati za chama cha upinzani nchini Kenya
Makala haya ya Wimbi la siasa, juma hili tunapigia darubini siasa za upinzani zinazoendelezwa nchini Kenya. Juma lililopita, kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, alitangaza kuitisha maandamano ya nchi nzima ndani ya siku 14 zijazo, ikiwa matakwa ya muungano wao wa Azimio hayatatekelezwa ikiwemo kushusha gharama ya maisha kwa raia.01/03/202309:54 -
Viongozi wa EAC wataka M23 kuachilia maeneo, viongozi wa AU wapinga mapinduzi Afrika
Makala ya Wimbi la siasa imeaangazia kauli ya viongozi wa EAC waliokutana huko Addis Ababa Ethiopia walithibitisha kuunga mkono michakato ya Luanda na Nairobi ambayo inawataka waasi wa M23 Huko DRC kusitisha mapigano na kuondoka katika maeneo wanayoyashikilia, katika sehemu ya pili viongozi wa Afrika walisisitiza msimamo wao wa kutovumilia njia zisizo za kidemokrasia, kuchukua madaraka wakijadili hali ya mapinduzi ya kijeshi kule Burkina Faso, Guinea, Mali na Sudan..Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka akiwa na wageni wake: Francois Alwende, mchambuzi wa siasa akiwa Nairobi nchini Kenya, pia Hajji Kaburu mchambuzi akiwa Dar Es Salaam Nchini Tanzania22/02/202310:08 -
Hatima ya usalama wa eneo la maziwa makuu na ule wa mashariki mwa DRC mashakani
Makala hii imeangazia hali inayoendelea huko mashariki mwa DRC ambapo hivi karibuni maelfu ya raia kwenye mji wa Goma, waliandamana kupinga uwepo wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanavyosema vimeshindwa kuwadhibiti waasi wa M23, ni maandamano ambayo yalifanyika siku chache baada ya viongozi wa Jumuia ya EAC kukutana jijini Bujumbura Burundi ambapo waliwataka waasi kusitisha mapigano, kuheshimisha mkataba wa Luanda unaowataka kuondoka katika maeneo wanayoyashikilia, wakati huu kundi hilo likiripotiwa kuchukua miji zaidi.08/02/202310:06 -
Joto la kisiasa limeanza kupanda nchini Kenya
Nchini Kenya siasa zimeanza tena miezi tano tu baada ya uchuguzi mkuu, siasa hizo zikichochewa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kukataa kutambua serikali ya rais William Ruto.Je hili lina maana gani ?Benson Wakoli, amezungumza na mchambuzi wa siasa za Kenya Brain Mutie katika makala haya ya wimbi la siasa.01/02/202310:00 -
UHUSIANO WA UFARANSA NA NCHI ZA BURKINA FASO NA MALI
Msikilizaji katika miaka ya hivi karibuni, nchi ya Ufaransa, imeendelea kujikuta matatani na mataifa ambayo wakati mmoja iliwahi kuyatawala wakati wa ukoloni. Hata hivyo hivi karibuni uhusiano kati ya baadhi ya nchi hizo na utawala wa Paris, umekuwa ukizorota kuanzia Mali na sasa Burkina Faso.25/01/202309:51
Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa