Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Nini maana ya maamuzi ya mahakama ya juu nchini Kenya na vipi wakenya wataendelea mbele.
Makala haya yanaangazia maana ya uamuzi wa mahakama ya upeo nchini Kenya ulioidhinisha ushindi wa William Ruto na nini kinastahili kutokea baada ya tukio hilo ili nchi kusonga mbele.07/09/202210:02 -
Uwakilishi wa wanawake katika Bunge la 13 nchini Kenya
Makala haya tunajadili safari ya kupigia upato uwakilishi wa wanawake katika mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika ,tukiangazia Bunge la 13 nchini Kenya.31/08/202210:38 -
Joto la siasa lapanda nchini Kenya
Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea uchaguzi Mkuu nchini Kenya, tunaendelea kukuarifu kinachoendelea kipindi hiki joto la kisiasa linapoendelea kupanda.Wageni wetu ni Ababu Namwamba kutoka muungano wa Kenya Kwanza, unaomuunga mkono mgombea urais William Ruto na Beatrice Elachi kutoka muungano wa mgombea mwingine Raila Odinga, kutoka muungano wa Azimio la Umoja.20/07/202209:48 -
Sudan: Jeshi latangaza kujiondoa kwenye mazungumzo ya kisiasa
Uongozi wa kijeshi nchini Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametangaza kuwa, jeshi linajiondoa kwenye mazungumzo ya kisiasa ili kutoa nafasi kwa viongozi wa kiraia kuunda serikali kufuatia mwendelezo wa maandamano. Je, jeshi linamaanisha katika uamuzi wake ? Tunachambua.08/07/202210:03 -
Waasi wa M 23 wauteka mji wa Bunagana baada ya makabiliano na jeshi la DRC.
Siku ya Jumatatu, Juni 13, waasi wa M 23 waliokuwa wanapambana na wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wameuteka mji wa Bunagana, ulio kwenye mpaka na Uganda. DRC inaishtumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao, madai ambayo Kigali inakanusha. Tunajadili.15/06/202209:55 -
Nafasi ya vijana kwenye siasa za Kenya
Nchini Kenya, joto la kisiasa linapoendelea kupanda kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti, tunaangazia nafasi na mchango wa vijana kisiasa lakini pia katika kuendeleza miji.01/06/202209:37 -
Mtoto wa rais Museveni aonesha nia ya kugombea uongozi wa Uganda
Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa rais Yoweri Museveni, ameonesha nia ya kuwania uongozi wa nchi hiyo.04/05/202209:58 -
Kenya: Nani atakuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga na William Ruto ?
Nchini Kenya, joto la kisiasa linaendelea kupanda kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwezi Agosti. Lakini je, wagombea wakuu wa urais Raila Odinga na William Ruto watawateua nani kuwa wagombea wenza ?20/04/202210:09 -
Maafisa wa usalama nchini Ethiopia watekeleza visa vya uhalifi wa kivita
Maafisa wa usalama nchini wametekeleza visa vya uhalifu wa kivita na ukiukwaji wa haki wa binadamu dhidi ya Watigray Kaskazini mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyotolewa na Mashirika mawili ya Kimataifa, Amnesty International na Human Rights Watch. Tunajadili hili.06/04/202210:00 -
Wasiwasi wa kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu nchini DRC mwaka 2023
Wiki hii tunaangazia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2023 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mashirika ya kiraia zaidi ya 60 za ndani na nje ya nchi hiyo, yanaonya kuwa, kuna dalilil za uchaguzi huo kucheleweshwa kama ilivyoshuhudiwa mwaka 2011 na 2018. Tunachambua na wanaharakati.23/03/202210:05 -
Kenya: Rais Uhuru Kenyatta amwidhinisha Raila Odinga
Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kumuunga mkono kiongozi wa upinzani wa muda mrefu Raila Odinga kuwa mrithi wake, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9. Hatua hii imekuja baada ya Kenyatta, kumtema naibu wake William Ruto ambaye amesema kiongozi huyo wa nchi, amemhadaa kisiasa. Tunachambua.17/03/202210:01 -
MJADALA: Vijana na Uongozi
Makala ya Wimbi la siasa juma hili, inaangazia Vijana na Uongozi, majadiliano haya yalifanyika mubashara (live) katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Nairobi, ambapo pia yalijumuisha wasikilizaji ambao walipata nafasi ya kuuliza maswali kwa wageni walioalikwa na mtayarishaji wa makala haya. Sikiliza zaidi...10/03/202209:54 -
Siasa za upinzani nchini Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu
Tunaangazia harakati za chama kikuu cha upinzani nchini Kenya Orange Democratic Movement (ODM), kutafuta uongozi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki, baada ya uchaguzi Mkuu mwezi Agosti.02/02/202210:13 -
Joto la kisiasa laendelea kupanda nchini Kenya kuelekea Uchaguzi wa Agosti
Tunaangazia joto la kisiasa, linaloendelea kupanda nchini Kenya, kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti mwaka huu. Wakenya watamchagua rais wao wa tano, baada ya Uhuru Kenyatta ambaye anaondoka madarakani.Kinyanganyiro kinatarajiwa kuwa kati ya kiongozi wa muda mrefu wa upinzani na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga na naibu rais William Ruto.19/01/202209:56 -
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok ajiuzulu
Tunaangazia hatua ya kujizulu kwa Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok wiki hii. Kujiuzulu kwa Hamdok kumekuja muda mfupi baada ya kurejeshwa kwenye nafasi hiyo, baada ya kuafikiana na uongozi wa kijeshi chini ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, aliyemwondoa madarakani mwezi Oktoba mwaka 2020.05/01/202210:18
Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa