Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
DRC: Viongozi wakutana Kinshasa kutathmini hali ya dharura Kivu Kaskazini na Ituri
Viongozi kutoka kwenye majimbo mawili ya Ituri na Kivu Kaskazini wanazungumza na wale wa Serikali kuu, kuhusu ikiwa makataa ya hali ya dharura iliyotangazwa kwenye majimbo yao iondolewe au la, ingawa wanasiasa wengi kutoka kwenye maeneo hayo wanataka iondolewe.16/08/202310:01 -
Mapinduzi ya Niger tumbo joto kwa ECOWAS
Nchini Niger viongozi wa mapinduzi wamekatakata kuonana na ujumbe wa ECOWAS kujadili mchakato wa kurejesha madarakani rais Mohamed Bazoum.09/08/202309:55 -
Juhudi za kikanda ili kukabiliana na mapinduzi ya kijeshi Afrika magharibi
Wimbi la siasa imeangazia yaliyojiri nchini Niger baada ya maafisa wa jeshi kumng’atusha madarakani Mohammed Bazoum aliyechaguliwa chini ya misingi ya kidemokrasia, hali inayoendelea kwa sasa pamoja na juhudi za Ecowass kutaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia, na kuachiwa huru kwa rais Bazoum. Kuchambua hili wachambuzi Mali Ali akiwa kwenye Visiwa vya Mayote, pamoja na Hajji Kaburu akiwa jijini Daresalaam nchini Tanzania.02/08/202309:59 -
Uchambuzi kuhusu siku mia moja za vitaa vya wenyewe kwa wenyewe Sudan
Katika Makala haya ya leo Ali Bilali anajadili na wachambuzi kuhusu siku mia moja ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan29/07/202310:02 -
Uchambuzi kuhusu siasa ya Zimbabwe baada ya upinzani kuzuiliwa kufanya kampeni
WImbi la siasa juma hili Ali Bilali na wachambuzi wake wanajadili hali ya kisiasa nchini Zimbabwe kuelekea kwenye uchanguzi mkuu wa rais27/07/202309:59 -
Maandamano ya upinzani nchini Kenya
Upinzani nchini Kenya umeitisha maandamano ya siku tatu wiki hii kupinga kile wanachosema ni kupanda kwa gharama ya maisha, ukitaka serikali ya rais William Ruto kushugulikia suala hilo kwa dharura.19/07/202309:44 -
Zimbabwe : Marafuku ya kuanzishwa kwa kampeni za chama cha upinzani
Tunaangazia hatua ya mahakama nchini Zimbabwe kuidhinisha marafuku kuanzishwa kwa kampeni iliyopangwa kufanywa na chama kikuu cha upinzani wakati huu pia kiongozi wake mkuu Nelson Chamisa akikabiliwa na vikwazo.15/07/202309:26 -
Hatua ya rais wa Senegal kutangaza kutowania muhula mwengine
Hatua hiyo rais Macky Sall, imesifiwa nje na ndani ya taifa lake baada ya kuwepo hofu kuwa angetangaza kuwania tena. Rueben Lukumbuka amezungumza na wachambuzi wa siasa kuhusu suala hili.06/07/202310:00 -
Siku ya Kimataifa ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili
Kuelekea siku ya Kimataifa ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili, watalaam Wanjohi Mugambi kutoka Kenya, na Pascal Baguez kutoka Ufaransa wanajadili maendeleo ya lugha hiyo.06/07/202310:07 -
Uasi wa kiongozi wa wapiganaji mamluki wa Wagner Yevgeny Prigozhin, nchini Urusi.
Juma hili msikilizaji tunatupia jicho matukio ya mwishoni mwa juma lililopita nchini Urusi, ambapo kiongozi wa kundi la wapiganaji, mamluki wa Wagner, Yevgeny Prigozhin, alitekeleza kitendo kilichotajwa kama uasi, baada yake kuongoza wapiganaji wake kuuteka mji wa Rostov-on-Don kusini, na kisha kusonga mbele kabla ya kusitisha mpango wao wa kufika Moscow.28/06/202310:00 -
Usalama nchini Uganda na ukanda baada ya mashambulio ya ADF
Kundi la waasi la ADF Lenye asili nchini Uganda ila limekuwa likitikileza mashambulio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,limewauwa watu 42 nchini Uganda baada ya kushambulia shule ya sekondari eneo la Kasese22/06/202310:04 -
Kamatakamata ya wapinzani kwenye mataifa ya Afrika nini hatma yake?
Makala ya wimbi la siasa hii leo inaangazia hali ya kamata kamata inayotekelezwa na vyombo vya usalama dhidi ya wapinzani kwenye mataifa kadhaa ya Afrika mfano huko DRC Salomon Idi Kalonda mshauri wa kisiasa wake Moise Katumbi, hali kama hiyo inashuhudiwa pia huko Burundi katika chama cha upinzani cha CNL, Nchini Senegal huko na Kinara wa Upinzani Ousmane Sonko alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kufuatia tuhuma za ubakaji. Mwandishi wetu Reuben Lukumbuka amewaalika Mali Ali ni mchambuzi wa siasa za Nchi za maziwa makuu akiwa Visiwani Mayotte na pia Francois Alwende ni mchambuzi na mataalamu wa siasa za DRC akiwa Jijini Nairobi nchini Kenya14/06/202310:01 -
Hatima ya mswada wa fedha nchini Kenya
Kwanini mswada wa fedha unazua gumzo na mjadala nchini Kenya ? Tunajadili hili kwenye Makala ya Wimbi la Siasa07/06/202310:02 -
Ziara ya rais Tshisekedi wa DRC huko CHINA,pia mchakato wa uchaguzi wa 2023
Makala ya wimbi la siasa wiki hii imeangazia ziara ya rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi nchini China, na pia maendeleo ya mchakato wa uchaguzi kwenye nchi hiyo.Waalikwa wetu katika kuzungumzia hili ni Kashando Mukanisa Yvon mchambuzi huru na mtaalamu wa siasa za DRC, wakili Moise Bashwira wa chama cha UNC moja ya vyama madarakani vya Sacred Union, na pia Muhindo Safari Akayezu wa chama cha upinzani cha Ensemble pour la République chake Moise Katumbi. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi31/05/202309:59 -
Hali inavyoendelea nchini Sudan
Makala ya wiki hii yanaangazia hali inavyoendelea nchini Sudan wakati huu kukiwepo na mkataba wa kusitisha mapigano24/05/202309:50
Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa