Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Tume huru ya Uchaguzi Kenya na mchakato wa kutangaza matokeo
Uchaguzi wa Kenya unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mchakato wa kutangaza matokeo huku Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya, IEBC ikijinadi kuwa ina mamlaka ya kutangaza matokeo ya mwisho licha ya matokeo kutangazwa katika vituo na majimbo ya kupigia kura. Unajua ni kwa nini IEBC inatoa msimammo huo? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kujua kwa undani.22/08/201710:01 -
Kampeni za lala salama zapamba moto nchini Kenya
Kampeni za lala salama nchini Kenya zimepamba moto kuelekea uchaguzi huo Agosti 8 mwaka huu huku wagombea Uhuru Kenyatta wa Chama cha Jubilei na mgombea wa NASA, Raila Odinga wakichuana vikali katika kinyang'anyiro hicho. Je nani atashinda katika uchaguzi huo na kwa nini? Uchambuzi wa kina katika Makala ya Wimbi la Siasa ukiwa naye Victor Robert Wile utakata kiu yako ya kujua mbivu na mbichi kuhusu uchaguzi wa Kenya.22/08/201710:19 -
Kenyatta achaguliwa tena Kenya upinzani wakimbilia mahakamani kupinga matokeo
Uchaguzi mkuu wa Kenya ulifanyika hivi karibuni na Rais Uhuru Kenyatta kutangazwa kuwa rais mteule lakini upande wa upinzani umekimbilia mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo ukidai kufanyika udanganyifu. Je nini mustakabali wa nchi ya Kenya baada ya uchaguzi huo? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kupata undani wa mada hiyo.22/08/201710:15 -
Umoja wa Mataifa waonya hali ya usalama Jamhuri ya Afrika ya Kati
Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulisema kuwa nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati inabiliwa na ombwe kubwa la kiusalama na kwamba jitihada zaidi zinahitajika ili kusaidia nchi hiyo kuepuka kurudi ilikotoka. Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kupata undani wa mada hii.19/06/201710:01 -
Uchaguzi DRC bado njia panda
Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia, DRC Joseph Kabila alisema kuwa hajawahi kuahidi kuwa uchaguzi utafanyika lini na akasisitiza kuwa uchaguzi bora utafanyika na si bora uchaguzi katika mazingira ya amani na usalama. Je wajua mustakabali wa uchaguzi wa DRC? ungana na Victor Robert Wile katika Makala haya ya Wimbi la Siasa kupata kinaga ubaga cha suala hilo.09/06/201709:59 -
Ufaransa watakavyomkumbuka Fraoncois Hollande
Francois Hollande aliyekua rais wa Ufaransa amemaliza muda wake na kuiaga Ikulu ya Ufaransa na kumwachia kijiti Rais mpya Emmanuel Macron ambaye sasa anachkua usukani wa kuiongoza nchi hiyo. Pamoja na kuondoka kwake Francois Hollande historia ya nchi hiyo itamweka katika kumbukumbu. Je rais huyo wa mstaafu atakumbukwa kwa yapi? Fuatilia Makala haya ya Wimbi la Siasa na Victor Robert Wile kupata undani wa mada hivyo.15/05/201710:10 -
Tofauti za kisiasa kumalizwa nchini Uganda
Serikali ya Sweden iko tayari kuingilia kati mvutano wa kisiasa nchini Uganda na kuwasuluhisha wanasiasa wanaotofautiana yaani Rais Yoweri Museveni na mpinzania wake Kiiza Besigye. Je jitahada hizo zinaweza kuwa mwarobaini kile kinachoendelea nchini Uganda? Ungana na Victor Robert Wile kupata undani wa mada hiyo katika Makala ya Wimbi la Siasa.03/04/201710:04 -
Serikali ya Burundi kugomea mazungumzo na hatima ya nchi
Mazungumzo ya amani ya Burundi yanaendelea kusuasua baada ya Serikali ya nchi hiyo kukataa kushiriki mazungumzo yaliyoitishwa Mjini Arusha na Mratibu wa usuluhishi na Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa. Nini hatima na mustakabali wa baadaye wa Burundi? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa hapa RFI Kiswahili kupata majibu ya swali hilo.17/02/201709:59 -
Rais mpya wa Gambia akabiliwa na changamoto
Rais mpya wa Gambia amerejea nchini mwake kutoka nchini Senegal alikokimbilia baada ya hali ya kisiasa kuchafuku wakati Yahya Jammeh alipogoma kuachia madaraka ya Urais baada ya kushindwa. Kutokana na hali hiyo Rais Adama Barrow anakabiliwa na changamoto lukuki za kiutawala. Ungana na Victor Robert Wile katika makala ya Wimbi la Siasa kufahamu mengi zaidi.02/02/201709:58 -
Obama na Trump watofautiana kiutawala
Kuondoka madarakani kwa Rais wa Marekani Barack Obama na kuingia madarakani kwa Donald Trump kumeibua mitizamo na hisia tofautitofauti miongoni mwa wananchi wa Marekani. Je sura ya Marekani kiutawala itaelekea katika mkondo gani baada ya utawala wa Obama kutamatika, ungana na Victor Robert Wile katika makala ya Wimbi la Siasa kupata undani mustakabali wa Marekani.16/01/201710:09 -
Makubaliano ya kisiasa kuivusha salama DRC?
Wanasiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC wamefikia makubaliano ya mchakato wa kipindi cha mpito kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwaka huu wa 2017 licha kuwepo changamoto mbalimbali. Je kusainiwa kwa makubaliano hayo kutaivusha DRC kutoka katika wimbi la ukosefu wa usalama na amani pamoja na mgogoro wa kisiasa? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kupata majibu ya swali hilo.06/01/201709:55 -
Rais Kenyatta adai mataifa ya kigeni yanaingilia siasa za Kenya
Rais Uhuru Kenyatta amesema mataifa ya kigeni, yanatumia fedha kufadhili mashirika ya kiraia kwa lengo la kuingilia siasa za Uchaguzi Mkuu mwaka 2017. Je, kuna ukweli katika hili ? Victor Abuso amezungumza na Mratibu Mkuu wa Mashirika ya kiraia nchini humo Suba Churchil akiwa jijini Nairobi.18/12/201609:56 -
Mazungumzo mapya ya kisiasa yaanza nchini DRC
Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limefanikiwa kuwaleta pamoja wapizani waliosusia mazungumzo ya awali ya kisiasa na wanasiasa wa serikali nchini humo kuhusu hatima ya rais Joseph Kabila.Je, mazungumzo haya mapya yatazaa matunda ?12/12/201609:39 -
Urusi yaitikisa mahakama ya ICC
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC ya mjini The Hague nchini Uholanzi imepata pigo jingine baada ya Urusi kutangaza kuondoa sahihi yake katika mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama hiyo. Swali linalobaki mezani hapa ni kwa nini Urusi imeamua kuchukua hatua hiyo? pata jibu la swali hilo ndani ya Makala ya Wimbi la Siasa na Victor Robert Wile.02/12/201610:00 -
Umoja wa Mataifa wahofia vita Sudani Kusini
Umoja wa Mataifa kupitia timu yake ya wataalam wa masuala ya haki za binadamu umesema kuwa unahofia nchi ya Sudani Kusini huenda ikatumbukia katika mauaji ya kimbari kama hatua hazitachukuliwa. Je unajua ni kwa nini Umoja wa Mataifa umeibua hofu hiyo? fuatilia Makala ya Wimbi la Siasa na Victor Robert Wile kupata undani wa mada hiyo.02/12/201610:00
Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa