Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Rais Samia Suluhu Hassan kukutana na viongozi wa upinzani
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kukutana na viongozi wa upinzani na kujadiliana nao kuhusu mustakabali wa kisiasa nchini humo baada ya baadhi yao kukimbia nchi na wengine kulalamikia kuminywa kwa misingi ya demokrasia. Je, itakuwaje ? Tunajadili01/05/202110:16 -
Kenya kutuma wanajeshi wake nchini DRC
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amesema Kenya imekubali kutuma wanajeshi wake Mashariki mwa nchi hiyo kusaidia katika vita dhidi ya ugaidi, kauli aliyotoa baada ya ziara ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jijini Kinshasa. Tunajadili.22/04/202110:12 -
Utovu wa usalama Mashariki mwa DRC
Utovu wa usalama linasalia suala tata Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kumekuwa na maandamano ya kutaka jeshi la Umoja wa Mataifa MONUSCO kuondoka nchini humo kwa kushindwa kuwainda raia. Tunajadili16/04/202110:24 -
Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Tanzania
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameagiza kufunguliwa kwa Televisheni za mitandaoni zilizofungiwa. Je, analeta mwamko mpya wa uhuru wa vyombo vya Habari nchini humo ? Tunajadili kwenye Makala ya Wimbi la Siasa.09/04/202110:06 -
Rais mpya wa Tanzania aahidi kupambana na ufisadi
Rais mpya wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewaahidi raia wake kuwa, hatokuwa na huruma na yeyote atakayehusika na wizi wa fedha za umma. Je, atafanikiwa katika changamoto hii ? Tunajadili.01/04/202110:15 -
Hali ya kisiasa Tanzania baada ya kifo cha John Pombe Magufuli
Upepo wa siasa nchini Tanzania, umechukuwa mkondo mpya baada ya kifo cha rais John Pombe Magufuli, kwenye makala haya Victor Robert Wile anaangazia hali kisiasa nchini humo baada ya kifo cha Magufuli.25/03/202110:02 -
Kifo cha rais wa Tanzania John Magufuli
Rais wa Tanzania John Magufuli amefariki dunia, baada ya kuugua ugonjwa wa moyo. Leo kwenye Makala haya, tunaangazia maisha ya Marehemu Magufuli.18/03/202110:18 -
Kundi la ADF latajwa kuwa la kundi la kigaidi
Marekani inasema kundi la waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la ADF, ni magaidi wizara ya Mambo ya nje ya Marekani ikisema viongozi wa makundi hayo, wanashirikiana kwa karibu na wale wa Islamic State na sasa wamekewa vikwazo.Victor Robert Wile anangaazia hatua hii katika makala haya.11/03/202110:12 -
Mvutano wa kisiasa nchini Uganda kati ya Bobi wine na rais Museveni
Makala ya juma hili la wimbi la siasa mwandishi wetu Victor Robert Wile, ameangazia siasa za Uganda, ambapo kiongozi wa upinzani, Robert Kygulanyi maarufu kama Wine, aliagiza mawakili wake kuondoa kesi ya kupinga ushindi wa rais Yoiweri Muveseni mahakama, kwa tuhuma mahakama kuegemea upande moja.26/02/202110:13 -
Matukio makubwa tuliyoyapa uzito mwaka 2019
Haya ndio makala ya mwisho ya Wimbi la Siasa mwaka 2019, tunaangazia matukio makubwa tuliyoyapa uzito kisiasa barani Afrika na kwingineko duniani.27/12/201909:24 -
Nini suluhu ya kisiasa kuhusu mzozo wa kuwavamia wageni nchini Afrika Kusini ?
Je, kuna suluhu ya kisiasa kuhusu mzozo wa wageni kuvamiwa na maduka yao kuvunjwa nchini Afrika Kusini ?Tunajadili hili katika Makala ya Wimbi la Siasa.06/09/201909:58 -
DRC yampata rais mpya, historia yaandikwa
DRC imempata rais mpya, Felix Thisekedi. Nchi hiyo ya Afrika ya Kati imeshuhudia ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya amani kwa mara ya kwanza tangu ilipopata uhuru mwaka 1960. Tunajadili hili kwa kina.26/01/201909:45 -
Tume ya Uchaguzi yahairisha Uchaguzi katika baadhi ya maeneo, Mashariki mwa DRC
Hatimaye, Uchaguzi Mkuu wa DRC utafanyika siku ya Jumapili, lakini Tume ya Uchaguzi imeahirisha zoezi hilo katika maeneo ya Butembo, Beni na Yumbi kwa sababu za kiusalama na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola.28/12/201809:57 -
Uchaguzi Mkuu wa DRC wahairishwa
Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 23 mwezi Desemba, sasa umeahirishwa hadi tarehe 30 baada ya kuteketea kwa ghala la kuhifadhi vifaa vya kupigia kura jijini Kinshasa.21/12/201809:23 -
Kampeni za DRC zakumbwa na vurugu
Siku 10 kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini DRC, mauaji yameripotiwa katika kampeni za siasa hasa katika mikutano ya Martin Fayulu, mgombea vya vyama upinzani lakini pia kuteketea moto kwa jengo la kuhifadhi vifaa vya kupigia kura jijini Kinshasa. Tunajadili hili kwa kina.15/12/201809:43
Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa