Pata taarifa kuu

Ukraine: Tume ya Ulaya yapendekeza msaada wa euro bilioni 50 kwa miaka minne

Tume ya Ulaya inapendekeza kwa nchi wanachama wa EU kutoa msaada kwa Ukraine wa euro bilioni 50 katika kipindi cha miaka minne ijayo, Rais wa tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, ametangaza leo Jumanne. Tunapendekeza hifadhi ya fedha kwa miaka minne ijayo ya euro bilioni 50. Hii inajumuisha mikopo na ruzuku, "afisa huyo amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen anashiriki katika tukio la Ubia kwa Miundombinu na Uwekezaji wa Kimataifa wakati wa mkutano wa kilele wa G7, katika Hoteli ya Grand Prince huko Hiroshima, Japani, Mei 20, 2023.
Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen anashiriki katika tukio la Ubia kwa Miundombinu na Uwekezaji wa Kimataifa wakati wa mkutano wa kilele wa G7, katika Hoteli ya Grand Prince huko Hiroshima, Japani, Mei 20, 2023. © REUTERS / JONATHAN ERNST
Matangazo ya kibiashara

"Tunapendekeza hifadhi ya kifedha kwa miaka minne ijayo ya euro bilioni 50. Hii inajumuisha mikopo na ruzuku,” mkuu wa serikali ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema katika mkutano na waandishi wa habari. Hifadhi hii itatoa "mtazamo" kwa Waukraine na "inapaswa pia kuhimiza wafadhili wengine kujitolea", ameongeza kiongozi huyo wa Ujerumani.

"Itaturuhusu kudhibiti msaada wetu wa kifedha kulingana na mabadiliko ya hali ya mambo, kwa sababu sote tunajua kuwa vita vinahitaji kubadilika zaidi kutoka kwetu", amebaini Rais wa Tume ya Ulaya.

Upanuzi huu wa bajeti ya mwaka wa 2021-2027 itabidi uidhinishwe kwa kauli moja na nchi wanachama, na kupokea idhini ya Bunge la Ulaya.

Bi von der Leyen pia amependekeza kuongezwa kwa bajeti ya Umoja wa Ulaya ya euro bilioni 15 kwa ajili ya usimamizi wa uhamiaji. Fedha hizi zitakusudiwa kusaidia nchi wanachama "kuimarisha udhibiti wa mpaka wetu wa nje" na ushirikiano na nchi za tatu, ameongeza.

Aidha, Rais wa Tume ameomba nyongeza ya euro bilioni 10 ili kuimarisha "ustahimilivu na ushindani" wa uchumi wa Ulaya. "Tuko katika ulimwengu tofauti kabisa na 2020 wakati bajeti ya kila mwaka ya Umoja wa Ulaya ilijadiliwa," amesema, akionyesha kuwa vita vya Ukraine na janga la Uviko vimeongeza mahitaji kwa kiasi kikubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.