Pata taarifa kuu

Georgia: Maandamano makubwa mbele ya Bunge baada ya kupitishwa kwa 'sheria ya Urusi'

Bunge la Georgia lilipitisha Jumatano Mei 1, 2024 kwa mara ya pili mswada wenye utata kuhusu "ushawishi wa kigeni", asili ya maandamano makubwa ya maandamano katika nchi hii ya Caucasia, yliyokandamizwa kwa nguvu na polisi. Wapinzani wake wanaiita "sheria ya Urusi". Jumanne jioni, Aprili 30, polisi walitawanya umati wa watu kwa kutumia maji ya kuwasha na mabomu ya machozi.

Maandamano dhidi ya "sheria ya Urusi" huko Tbilisi baada ya kupitishwa kwa usomaji wa pili wa sheria hii, Mei 1, 2024.
Maandamano dhidi ya "sheria ya Urusi" huko Tbilisi baada ya kupitishwa kwa usomaji wa pili wa sheria hii, Mei 1, 2024. © Irakli Gedenidze / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Makumi ya maelfu ya waandamanaji walikusanyika tena huko Georgia Jumatano jioni kupinga mswada wenye utata kuhusu "ushawishi wa kigeni", uliopitishwa katika hatua ya pili na Bunge. Maandamano haya yanahamasisha watu wa Georgia. Wakati huu, maandamano yalionekana kuwa makubwa kuliko kawaida, kulingana na mwandishi wetu huko Tbilisi, Régis Genté.

Kura hii iliamsha hasira ya wakazi wa Georgia, ambao walikusanyika mbele ya Bunge. Saa nne usiku kwa saa za ndani, kulikuwa na mkusanyiko mkubwa kutoka sehemu kadhaa za nchi, sio mji mkuu tu kama katika maandamano ya hapo awali.

Kuna hisia ya wakati wa kihistoria ambayo inashikiliwa na sehemu nzima ya watu wanaokataa sheria hii ambayo wanaiita "sheria ya Urusi". Siku ya Jumatano, mvutano ulikuwa zaidi ya hapo awali kati ya serikali, ambayo inataka kabisa kupitisha sheria, kama Waziri Mkuu Irakli Kobakhidzé alivyotukumbusha tena mchana, na sehemu ya watu, ambao wanakataa sheria hii.

Kwa hiyo kulikuwa na umati uliodhamiria kutotoka mitaani hadi muswada huu utakapoondolewa.

Kura 83 kati ya 150

Hapo awali, wabunge walipigia kura rasimu hii kwa kura 83 za ndio na 23 za hapana ambayo chama tawala cha Georgian Dream cha oligarch Bidzina Ivanishvili kinataka kupitisha kwa uhakika katikati ya mwezi wa Mei, licha ya wiki tatu za uhamasishaji katika mitaa ya wapinzani wa muswada huo. Nakala hii, iliyochochewa sana na sheria ya Urusi ya mwaka 2012, inapanga kulazimisha mashirika ya kiraia na vyombo vya habari kujitangaza kuwa "mawakala wa kigeni" ikiwa zaidi ya 20% ya bajeti yao inatoka nchi nyingine.

Mchana wakati wa mijadala, kulizuka makabiliano kati ya wabunge katika Bunge la Georgia wakati wa kikao cha kutathmini sheria hiyo. Katika picha zilizorushwa na televisheni ya Georgia, kuliweza kuonekana mbunge akirusha kitabu kuelekea kwa wabunge wa upinzani, huku wengine wakikabiliana wao kwa wao wakipigana makonde.

Nakala lazima isomwe mara tatu katika Bunge na kuridhiwa na rais. Rais wa Georgia anatarajiwa kupiga kura ya turufu, lakini chama tawala kina viti vya kutosha bungeni kuibatilisha. Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel alizingatia kwamba maandishi hayaendani na matakwa ya Georgia ya kuwa mwanachama wa EU.

Siku ya Jumatano, Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, alisema kuwa alikuwa akifuatilia kwa "wasiwasi mkubwa" maandamano huko Georgia yaliyokandamizwa na polisi, kulaani "vurugu" na kuitaka Tbilisi "kuwa tumivu" kuelekea Umoja wa Ulaya .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.