Pata taarifa kuu

Marekani: Bunge la Seneti lapigia kura msaada kwa Ukraine, bilioni moja ya vifaa kutumwa

Baada ya miezi kadhaa ya kizuizi, Bunge la Marekani limepitisha hatua za usalama za kitaifa zilizoombwa na Ikulu ya White House. Bunge la Seneti limeidhinisha rasimu hiyo kwa wingi mkubwa, na msaada wa kijeshi kwa Ukraine hasa utaweza kutolewa.

Capitol, Makao makuu ya Bunge la Congress (Baraza la Wawakilishi na Seneti) , huko Washington.
Capitol, Makao makuu ya Bunge la Congress (Baraza la Wawakilishi na Seneti) , huko Washington. AP - J. Scott Applewhite
Matangazo ya kibiashara

"Nitatia saini rasmu haii na kuhutubia watu wa Marekai mara tu itakapofika kwenye meza yangu. " Joe Biden hakungoja muda mrefu wa kujipongeza baada ya Bunge la Seeti kuidhinisharasimu hiyo ambayo kwa hivyo ataitangaza leo Jumatano, Aprili 24.

Mpango wa msaada wa dola bilioni 95 wa Marekani, unaojumuisha fedha kwa ajili ya Israel, Taiwan na kauli ya mwisho kwa TikTok, ulipata uungwaji mkono mkubwa katika Bunge la Seneti la Marekani. "Mwishowe, hatimaye, hatimaye. Usiku wa leo, baada ya zaidi ya miezi sita ya kufanya kazi kwa bidii, na misukosuko mingi, Marekai inatuma ujumbe kwa ulimwengu mzima: hatutawapa kisogo,” almepongeza kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, Chuck Schumer.

Umuhimu uliishia kuwa sheria

Matokeo ya haraka zaidi ni kwamba misaada ya Marekani kwa Ukraine, iliyozuiwa tangu mwanzoni mwa mwaka, itaweza kuanza tena haraka sana: kati ya dola bilioni 60 zilizotolewa kwa maandishi, vifaa bilioni moja vitatumwa kwa siku chache zijazo, ifikapo mwisho wa juma kwa ajili ya dharura zaidi.

Jeshi la Marekani limekuwa likijiandaa kwa muda mrefu, na kinachobakia ni kuhifadhi tu usafiri wa kupeleka risasi za Marekani nchini Ukraine, hasa kwa silaha ambazo nchi hiyo imenyimwa tangu mwanzo wa vita. Vifaa hivi vitachukuliwa moja kwa moja kutoka kwa hifadhi ya jeshi la Marekani.

Katika awamu hii mpya ya msaada mkubwa unaojadiliwa na mamlaka ya Ukraine, pia kuna silaha za kupambana na ndege kukabiliana na mashambulizi ya anga ya Urusi. Ajabu ni kwamba katika usafirishaji unaofuata, nakala hii inabaini kwamba kutakuwa na makombora ya masafa marefu ambayo jeshi la Marekani hadi sasa limesita kutoa ili lisichokoze Urusi.

Lakini hali kwenye uwanja wa vita ni ngumu sana kwa jeshi la Ukraine kwamba umuhimu uliishia kuwa sheria. Katika mitandao ya kijamii, Volodymyr Zelensky amesema "anashukuru Bunge la Seneti la Marekani kwa kuidhinisha msaada muhimu kwa Ukraine."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.