Pata taarifa kuu
WAHAMIAJI-HAKI

Wahamiaji kupelekwa Rwanda: Baraza la EU na UN waitaka Uingereza kurejelea sheria yake

Usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, mabunge yote mawili ya Uingereza yameidhinisha mswada wa sheria unaoruhusu kufukuzwa kwa waomba hifadhi walioingia kinyume cha sheria nchini humo na kupelekwa nchini Rwanda.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Rais wa Rwanda Paul Kagame  wanakutana kwa mazungumzo katika 10 Downing Street, London, Uingereza, Alhamisi Mei 4, 2023.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Rais wa Rwanda Paul Kagame wanakutana kwa mazungumzo katika 10 Downing Street, London, Uingereza, Alhamisi Mei 4, 2023. © Stefan Rousseau / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Haki za Binadamu katika Barazala la Umoja wa Ulaya ametoa wito leo Jumanne kwa serikali ya Uingereza kurejelea muswada huu wa sheria wa kuwafukuza wahamiaji kwenda nchini Rwanda, baada ya mabunge mawili kupigia kura muswada huo

"Serikali ya Uingereza inapaswa kujizuia kuwafukuza watu kufuatia mpango wake wa kuwapeleka nchini Rwanda na kurejelea kuhusu ukiukwaji wa uhuru wa mahakama dhidi ya muswada huo wa sheria ", amesema Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Baraza la Ulaya, Michael O’Flaherty. London ni sehemu ya taasisi hii inayoundwa na nchi 46 wanachama.

Umoja wa Mataifa umetoa wito kama , ukiitaka serikali ya Uingereza kurejelea mpango wake wa kuwafukuza waomba hifadhi na kuwapeleka nchini Rwanda

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.