Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE- MAPIGANO

EU kuendelea kuisaidia Ukraine kupambana na Urusi

Rais wa kamisheni ya umoja wa Ulaya, Ursula von de Leyen, ameahidi umoja huo kuendelea kuisaidia Ukraine kwa vifaa vya kisasa vya kijeshi, wakati huu taifa hilo likiendelea  kushambuliwa na Urusi.

Ursula Von De Leyen, Rais wa EU
Ursula Von De Leyen, Rais wa EU © AP / Jean-Francois Badias
Matangazo ya kibiashara

Akihutubia mkutano wa jukwaa la kiuchumi mjini Davos, Uswis, Von de Leyen, amesema kamwe hawatorudia nyuma kuisaidia Ukraine, akionya mwishowe haki itapatikana.

“Kwa karibu mwaka mmoja sasa, Ukraine imeushangaza ulimwengu, wakati huu uvamizi ulipoanza.” amesema Ursula Von De Leyen.

Rais wa Ukraine amekuwa ameendelea kuyataka mataifa ya magharibi kumpa silaha zaidi ilikupigana na uvamizi wa Ukraine nchini mwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.