Pata taarifa kuu

Mkuu wa EU, Ursula von der Leyen kuzuru Ukraine Jumanne ya wiki hii

NAIROBI – Mkuu wa tume ya umoja wa ulaya EU, Ursula von der Leyen, atazuru Kyiv siku ya Jumanne ya wiki hii kwa ajili ya mazungumzo na rais Volodymyr Zelensky, imesema taarifa ya msemaji wa EU.

Ursula von der Leyen , Mkuu wa EU
Ursula von der Leyen , Mkuu wa EU REUTERS - JOHANNA GERON
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Eric Mamer msemaji wa tume ya umoja wa ulaya, mkutano kati ya viongozi hao wawili utagusia kila sehemu ya uhusiano kati ya tume hiyo na Ukraine.

Ziara hii imetajwa kuwa njia moja ya tume hiyo kuonyesha mshikamano kati yake na Kyiv ambayo imeshambuliwa na jirani yake Urusi.

Hii itakuwa mara ya tano kwa von der Leyen kutembelea nchi ya Ukraine tangu Urusi ilipoaanzisha mashambulio nchini humo mwezi Februari mwaka uliopita.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy na rais wa tume ya umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, jijini Kyiv Ukraine, Tarehe  2 Februari 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy na rais wa tume ya umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, jijini Kyiv Ukraine, Tarehe 2 Februari 2023. via REUTERS - UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS SER

Kutokana na hatua ya Urusi kuendelea kuishambulia kwa makombora nchi yake Ukraine, ziara ya mkuu huyo wa EU inatarajiwa kufanyika chini ya ulinzi mkali, hii ikiwa sababu ya tume hiyo kutotoa maelezo zaidi na ratiba ya ziara hiyo.

Ziara hii pia inatarajiwa kufanyika Kuelekea siku ya kukumbuka ya ushindi wa jeshi la kisovieti dhidi ya wanajeshi kinazi kutoka Ujerumani.

Tume ya umoja wa ulaya imeendelea kuituhumu Urusi kwa kuishambulia Ukraine, mshirika wa mataifa ya Magharibi, EU ikiwa tayari imetangaza vikwazo kwa maofisa wa serikali ya Urusi na wafanyabiashara wanaohusishwa na vita vinavyoendelea nchini Ukraine.

Urusi imerusha makombora nchini Ukraine usiku wa kuamkia Jumatatu ya tarehe 8 ya mwezi Mei mwaka huu wa 2023
Urusi imerusha makombora nchini Ukraine usiku wa kuamkia Jumatatu ya tarehe 8 ya mwezi Mei mwaka huu wa 2023 REUTERS - VALENTYN OGIRENKO

Urusi pia imetekeleza mashambulio ya makombora nchini Ukraine, Kuelekea siku hiyo ya kukumbuka ushindi wa jeshi la kisovieti dhidi ya wanajeshi kinazi kutoka Ujerumani.

Urusi imekuwa ukionya nchi za Magharibi kutokana na juhudi zake za kuendelea kuihami Ukraine, ikisema kuwa hatua hiyo itachochea mzozo kati yake na Ukraine zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.