Pata taarifa kuu

Bunge la Uingereza lapitisha mswada wa kuwafukuza wahamiaji na kuwapeleka nchini Rwanda

Bunge la Uingereza limeidhinisha usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne mswada tata wa kuwafukuza nchini Uingereza na kuwapeleka nchini nchini Rwanda waomba hifadhi walioingia Uingereza kinyume cha sheria. London inataka kuzindua safari zake za kwanza za ndege kwenda Rwanda mwezi Julai.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak, akiwa mbele ya Bunge Jumatatu Oktoba 16, 2023.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak, akiwa mbele ya Bunge Jumatatu Oktoba 16, 2023. via REUTERS - UK PARLIAMENT/Maria Unger
Matangazo ya kibiashara

Mabunge yote mawili ya a Uingereza hatimaye yaMEidhinisha mswada huo, baada ya hekaheka ya nenda rudi. Bunge limeidhinisha usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne muswada unaoruhusu kufukuzwa nchini Uingereza na kupekwa nchini Rwanda waomba hifadhi ambao waliingia nchini Uingereza kinyume cha sheria, baada ya vita visiyoisha kati ya mabunge yote mawili.

Mswada huo unaielezea Rwanda kuwa nchi salama na sehemu muhimu ya mipango ya serikali ya kuwapeleka baadhi ya watu wanaotafuta hifadhi Uingereza.

Mswada huo umekosolewa vikali na vyama vya upinzani lakini baada ya mijadala kadhaa wabunge wa Uingereza (the Lords) walitupilia mbali pingamizi zao dhidi yake Jumatatu jioni.

Waziri wa Mambo ya Ndani James Cleverly alisema kupitisha mswada huo ni "wakati wa kihistoria katika mpango wetu wa kuzuwia mashua."[za wahamiaji kuingia Uingereza].

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesema safari za ndege za kuelekea Rwanda zitaanza ndani ya wiki 10 hadi 12, baada ya kushindwa lengo lake la awali ambapo safari hizo zilitarajiwa kuanza kati ya mwezi wa Septemba na Desemba mwaka jana.

Lakini safari za kuondoka bado zinaweza kusimamishwa na mahakama au kucheleweshwa kwa ajili ya kupata ndege ambazo zitatumiwa kuwasafirisha wahamiaji hao hadi Rwanda.

Baada ya pingamizi nyingi, kupitishwa kwa mswada huo kulikuwa ni ushindi wa kisiasa kwa Rishi Sunak.

Huku uchaguzi mkuu ukikaribia, waziri mkuu hana muda mrefu wa kuthibitisha iwapo mpango wake utafanya kazi kwa ufanisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.