Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE- MAPIGANO

Urusi yazituhumu nchi za Magharibi kwa kujaribu kuiharibu

Urusi imezituhumu nchi za magharibi kwa kujaribu kuiharibu kabisa nchi hiyo, Moscow ikitoa maneno makali dhidi ya mkuu wa kamisheni ya umoja wa Ulaya, Ursula von De Leyen, ambaye yuko mjini Kiev, Ukraine.

kamisheni ya umoja wa Ulaya, Ursula von De Leyen amefanya ziara nchini Ukraine
kamisheni ya umoja wa Ulaya, Ursula von De Leyen amefanya ziara nchini Ukraine via REUTERS - UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS SER
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya Von De Leyen nchini Ukraine, imekuja wakati ambapo rais Vladmir Putin, akihudhuria sherehe za maadhimisho ya kumalizika kwa vita ya pili ya dunia, kusini wa Urusi, ikiwa ni kumbukizi ya ushindi wa taifa hilo la  kisoevieti dhidi ya utawala wa Kinazi wa Ujerumani.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, amedai kuwa umoja wa Ulaya na hasa Ursula Von Deleyen, ameshatamka wazi kuwa ni lazima Urusi ishindwe ili uchumi wake utatizike.

Matamshi ya Urusi, yamekuja saa chache tangu Von de leyen, aandike kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, kuwa amewasili mjini Kiev, tayari kwa mkutano ulioitishwa na Ukraine, ambayo inataka kuwa mwanachama wa umoja huo.

Kwa majuma kadhaa umoja wa Ulaya, umekuwa ukisisitiza kuwa Urusi lazima ikabiliwe vilivyo, huku nchi wanachama zikitangaza misaada zaidi ya kijeshi kwa Ukraine.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.