Pata taarifa kuu

Mazishi ya kihistoria : Waingereza watoa heshima za mwisho kwa malkia Elizabeth

Nchini Uingereza, mazishi ya Malkia Elizabeth wa pili, aliyefariki dunia tarehe nane mwezi huu, akiwa na umri wa miaka 96 yanafanyika leo jijini London. Wananchi wa taifa hilo wameungana na wengine duniani kuaga mwili wa Malkia Elizabeth wa pili aliyeongoza kwa kipindi kirefu cha miaka 70 tangu mwaka 1952. 

Jeneza la Elizabeth II linaingizwa katika Kanisa la St. George's huko Windsor, Septemba 19, 2022.
Jeneza la Elizabeth II linaingizwa katika Kanisa la St. George's huko Windsor, Septemba 19, 2022. © AP/Kirsty Wigglesworth
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya watu, wakiwemo viongozi mbalimbali duniani wakiongozwa na rais wa Marekani Joe Biden, mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron na marais kutoka barani Afrika wameshuhudia mazishi hayo. 

Katika barabara za jiji la London, msafara wa kijeshi uliobeba mwili wa Malkia Elizabeth wa pili, ulipitishwa kwa mara ya mwisho, kwa watu kutoa heshima zao za mwisho. 

Awali, shughuli za mazishi zilianzia katika Kanisa kuu la Westminster Abbey ambako viongozi mbalimbali walihudhuria ibada, katika Kanisa alikofunga ndoa, akatawazwa kuwa Mfalme na sasa ibada ya mazishi. 

Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby katika mahubiri yake, alimkumbuka Malkia Elizabeth wa pili kama Mtumishi wa watu, katika kipindi chote cha uhai wake. 

Malkia Elizabeth wa pili, amezikwa Pembeni mwa  kaburi la baba yake Mfalme George wa Sita, Mama yake Malkia Elizabeth, dada yake Margaret katika Kanisa la Mtakatifu George, huko Windsor Castle.  

Mwili wa mume wake, Mwanamfalme Philip aliyefariki dunia mwaka uliopita, akiwa na umri wa miaka 99, unatarajiwa pia kuzikwa pamoja na mke wake. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.