Pata taarifa kuu

Mfalme Charles III aahidi kufuata nyayo za Elizabeth II

Mfalme Charles III amejitokeza kwa mara ya kwanza mbele ya Bunge, lililokutana katika kongamano katika Ukumbi wa Kasri la Westminster Jumatatu, Septemba 12. Alipokea rambirambi kutoka kwa Wabunge na Watu maarufu, kisha alihutubia wabunge. Hata hivyo mfalme anatarajiwa nchini Scotland kwa ajili ya sherehe nyingine za mazishi.

Mfalme Charles III akitoa hotuba yake kwa Camilla, Malkia, katika Ukumbi wa Westminster, ambapo Mabunge mawili yalikutana kutoa rambirambi zao, kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II, huko London, Jumatatu Septemba 12, 2022 .
Mfalme Charles III akitoa hotuba yake kwa Camilla, Malkia, katika Ukumbi wa Westminster, ambapo Mabunge mawili yalikutana kutoa rambirambi zao, kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II, huko London, Jumatatu Septemba 12, 2022 . AP - Dan Kitwood
Matangazo ya kibiashara

Mfalme mpya Charles III amehutubia mbele ya Wabunge na viongozi wakuu maarufu wa Bunge, Maspika wa Mabunge yote mawili, Lord McFall na Lindsay Hoyle, wakiwasilisha kwake rambirambi kwa Elizabeth II. "Alikuwa kiongozi, na mtumishi, wa watu wake," Spika McFall amesema. Unyenyekevu na uadilifu wake ulionyesha heshima. Mheshimiwa, kwa niaba ya baraza lakitaifa, ninaahidi uaminifu wangu kwako. Β»

"Tunajua kwamba utachukua majukumu yenye ujasiri na heshima iliyoonyeshwa na marehemu Malkia," amehakikishia Lindsay Hoyle.

Tangu kutangazwa kwa kifo cha Malkia aliyekuwa na miaka 96 kilichotokea katika Kasri la Balmoral nchini Scotland, misururu ya mipango imekuwa ikiendelea ya kumuaga Malkia huyo aliyeiongoza Uingereza kwa miaka 70.Β 

Katika tamko lake la kwanza hadharani tangu kufariki kwa bibi yake, Mwanamfalme Harry amesema Malkia Elizabeth atakoswa sio tu na familia yake lakini pia dunia nzima kwa ujumla. Malkia anatarajiwa kuzikwa tarehe 19 Septemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.