Pata taarifa kuu

Malkia Elizabeth II: Mazishi ya kitaifa kufanyika leo London

Wakuu wa nchi na serikali kote ulimwenguni wanajiunga tangu jana Jumapili na wananchi wa Uingereza kutoa heshima za mwisho kwa Malkia Elizabeth II, aliyefariki dunia siku chache zilizopita. Mazishi ya kihistoria yanafanyika leo Jumatatu.

Jeneza la Malkia Elizabeth II linaondoka Westminster Abbey baada ya hafla ya kwanza ya mazishi mnamo Septemba 19, 2022 huko London.
Jeneza la Malkia Elizabeth II linaondoka Westminster Abbey baada ya hafla ya kwanza ya mazishi mnamo Septemba 19, 2022 huko London. © AP/Dominic Lipinski
Matangazo ya kibiashara

Wakuu wa nchi kutoka kote ulimwenguni wamekuwa wakiwasili kuungana na washiriki wa familia ya Kifalme kukumbuka maisha na huduma ya Malkia.

Wanasiasa wakuu wa Uingereza na mawaziri wakuu wa zamani pia watakuwepo.

Wanachama wa familia za kifalme kutoka kote Ulaya, ambao wengi wao walikuwa ndugu wa damu wa Malkia wanatarajiwa - Mfalme Philippe wa Ubelgiji na Malkia Mathilde na Mfalme Felipe wa Uhispania na Malkia Letizia watakuwa huko.Pia viongozi mbalimbali kutoka Afrika tayari wamewasili

Kipindi cha maombolezo ya taifa kinamalizika nchini Uingereza. Malkia Elizabeth II, ambaye alifariki dunia mnamo Septemba 8 akiwa na umri wa miaka 96, atazikwa alasiri hii Jumatatu. Jana Jumapili, maelfu ya watu waliendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa malkia.

Mwili utasafirishwa kwanza hadi Westminster Abbey kwa ibada ya kidini mbele ya maelfu ya watu, na kisha kuelekea kasri la Windsor kwa ibada ya ki familia na watu wa karibu zaidi, hatimaye, maziko ya kibinafsi.

Itakuwa siku ya hisia mbalimbali ikiwemo huzuni kubwa, Hali ambayo haijashuhudiwa tangu mazishi ya mwisho ya kitaifa, yale ya Winston Churchill, karibu miaka 60 iliyopita.

Kutoka Westminster Abbey, milango itafunguliwa kwa wageni kuanza kuwasili kabla ya ibada ya kidini mapema leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.