Pata taarifa kuu

Uingereza: Mazishi ya Malkia Elizabeth II yatafanyika Septemba 19

Mazishi ya Malkia Elizabeth II, ambaye alifariki dunia Alhamisi huko Scotland, yatafanyika Jumatatu Septemba 19 huko London, Kasri la Buckingham lilmetangaza Jumamosi. Viongozi kutoka kote ulimwenguni wanatarajiwa kwa mazishi hayo, yatakayofanyika Westminster Abbey saa tano mchana kwa saa za huko (sawa na saa sita mchana saa Paris). Mfalme Charles III, mwanawe aliyemrithi, ametangaza likizo ya umma nchini Uingereza kwa hafla hiyo

Kabla ya hafla hiyo, mwili wa Malkia Elizabeth II utaonyeshwa hadharani kwa siku nne katika Ukumbi wa Westminster Hall, sehemu kongwe zaidi ya Bunge, baada ya kupitishwa katika mitaa ya London.
Kabla ya hafla hiyo, mwili wa Malkia Elizabeth II utaonyeshwa hadharani kwa siku nne katika Ukumbi wa Westminster Hall, sehemu kongwe zaidi ya Bunge, baada ya kupitishwa katika mitaa ya London. © AP Photo/Alberto Pezzali
Matangazo ya kibiashara

Mazishi yatafanyika huko London Westminster Abbey, ambapo wafalme na malkia kadhaa wa Uingereza wanapumzika.

Viongozi kutoka kote ulimwenguni wanatarajiwa kwa mazishi haya. Miongoni mwa watu wanaotarajiwa, marais wa Marekani Joe Biden na wa Ufaransa Emmanuel Macron, mfalme wa Japan, Naruhito, pamoja na viongozi wengi wa makoloni ya zamani ya Uingereza.

Kabla ya hafla hiyo, mwili wa Malkia Elizabeth II utaonyeshwa hadharani kwa siku nne katika Ukumbi wa Westminster Hall, sehemu kongwe zaidi ya Bunge, baada ya kupitishwa katika mitaa ya London.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.