Pata taarifa kuu

Mazishi ya Elizabeth II: changamoto kubwa ya usalama kwa polisi wa London

Mazishi ya Malkia mnamo Jumatatu Septemba 19 yanatazamiwa kuwa zoezi kubwa zaidi kuwahi kusimamiwa na polisi wa London. Ili kuhakikisha tukio linaendelea vizuri na kuzuia matukio yanayoweza kusababishwa na umati wa watu, idadi kubwa ya maafisa wa polisi imewekwa na zaidi ya maafisa wa polisi 10,000 watakuwa tayari kusimamia zoezi hilo.

Maafisa wa polisi wamewekwa kando ya Barabara ya Mall inayoelekea Buckingham Palace hadi Westminster Hall, ambapo jeneza la Malkia linaonyeshwa hadi mazishi yake Jumatatu Septemba 19.
Maafisa wa polisi wamewekwa kando ya Barabara ya Mall inayoelekea Buckingham Palace hadi Westminster Hall, ambapo jeneza la Malkia linaonyeshwa hadi mazishi yake Jumatatu Septemba 19. AP - Kirsty Wigglesworth
Matangazo ya kibiashara

Huku wageni 2,000 wakitarajiwa katika eneo la Westminster Abbey kwa mazishi ya Malkia, wakiwemo wakuu wa nchi 500 kutoka duniani kote, mazishi hayo yatakuwa changamoto kubwa ya usalama kwa vikosi vya usalama. Idadi kubwa ya maafisa wa polisi kwa siku moja muhimu zaidi kuliko wakati wote wa Michezo ya Olimpiki mnamo 2012.

Makumi ya maelfu ya wageni wanatarajiwa kufanya safari siku ya Jumatatu, huku Waingereza wakiendelea kujipanga kwenye foleni isiyoisha kutoa heshima zao mbele ya jeneza la malkia.

Polisi itaweka kilomita 36 za vizuizi na maafisa 10,000 wa usalama watatumwa katika mji mkuu wa Uingereza, kulingana na Gazeti la The Guardian. Ili kukabiliana na ukubwa wa tukio hilo, maafisa wa polisi kutoka kote nchini wameitwa. Vitengo mbalimbali vya jeshi na polisi, ikiwa ni pamoja na kitengo cha baharini pia wanahitaji kuajiriwa, kama alivyosema Naibu Kamishna Stuart Cundy.

Amebaini kwamba ameanzisha itifaki sahihi ya kudhibiti umati na kuzuia jaribio lolote la shambulio au vurugu. "Vifaa na teknolojia tuliyo nayo, ili tuweze kuona kila kitu kinachotokea kutoka pembe tofauti, ni muhimu kabisa katika suala la udhibiti wa umati," amesema, kulingana na shirika la habari la AFP. Maafisa wa polisi wataandamana na helikopta, na maafisa wanaoongoza operesheni kutoka kwenye chumba maalumu cha ukaguzi. Ndege zisizo na rubani zitapigwa marufuku katika mji mkuu mzima.

Wakuu wa Nchi kusindikizwa wakiwa katika mabasi

Emmanuel Macron, Rais wa Marekani Joe Biden, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, mwenzake wa Australia Anthony Albanese, Mfalme wa Japan Naruhito na viongozi wengine wengi wamethibitisha kuhudhuria mazishi ya malkia Elizabeth II.

Isipokuwa kwamba katika hati zilizotumwa Jumamosi, Septemba 10 kwa balozi, Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza inapendekeza kwamba wakuu wa nchi wasafiri hadi Westminster Abbey na mabasi yaliyokodishwa kwa hafla hiyo, badala ya magari ya kibinafsi, kwa sababu ya "vizuizi vikali vya usalama barabarani". Kama ilivyoonyeshwa na vyombo vya habari vya Marekani Politico, ambavyo viliweza kuangalia hati hizi, uwanja wa ndege wa Heathrow wa London hautapokea ndege za kibinafsi kama hatua ya usalama, ambayo italazimika kutua katika "viwanja vya ndege visivyo na watu mara kwa mara".

Haki ya kuandamana itaheshimiwa

Baada ya shambulio la visu dhidi ya maafisa wawili wa polisi katikati mwa mji wa London siku ya  Ijumaa Septemba 16, maafisa wa polisi wanabaki macho zaidi katika maandalizi ya mazishi.

Kutokana na maandamano yanayowezekana pembezoni mwa maandamano hayo, Stuart Cundy anaeleza kuwa kila afisa wa polisi atalazimika kuheshimu haki ya kuandamana. "Tumehakikisha kwamba kila afisa wetu wa polisi aliyetumwa London anaelewa kuwa watu wana haki ya kuandamana. Mwitikio wetu utalazimika kuwa sawia, uwiano, na maafisa wetu watachukua hatua ikibidi tu,” ameongeza.

Naibu Mkuu wa polisi ya Thames Valley, Konstebo Tim De Meyer almesema maafisa watatumia uamuzi wao bora. "Tunajua tunapaswa kusawazisha uhuru wa kujieleza na usalama wa umma. Tutakuwa makini kusawazisha haya mawili na kuheshimu hadhi ya tukio hili. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.