Pata taarifa kuu

Jeneza la Malkia Elizabeth II laanza safari ya mwisho

Mazishi yatafanyika Septemba 19 Westminster Abbey huko London, kitovu cha harusi za kifalme, kutawazwa na mazishi kwa karibu milenia moja.

Mamia ya watu walijipanga barabarani huku gari la kubebea maiti lililobeba jeneza la Malkia Elizabeth wa Uingereza likipita katika kijiji cha Ballater, karibu na Balmoral, Scotland.
Mamia ya watu walijipanga barabarani huku gari la kubebea maiti lililobeba jeneza la Malkia Elizabeth wa Uingereza likipita katika kijiji cha Ballater, karibu na Balmoral, Scotland. AP - Andrew Milligan
Matangazo ya kibiashara

Malkia Elizabeth II ameanza safari yake ya mwisho Jumapili, jeneza lake likiondoka kwenye Kasri la Balmoral kuelekea Edinburgh, kabla ya kurejea London Jumanne na mazishi yake ya kiserikali kufanyika mnamo Septemba 19.

Gari la kubebea maiti la kifalme, la kwanza kati ya msafara wa magari saba, limevuka lango la makazi hayo ambapo malkia alipenda kutumia majira ya kiangazi baada ya saa 10:00 asubuhi kwa barabara.

Jeneza la mwaloni lilifunikwa na kitambaa cha kifalme cha Scotland ambacho kilikuwa kimewekwa shada la maua. Mwili wake ulikuwa unatarajiwa kuwasili Edinburgh, mji mkuu wa Scotland, karibu saa kumi alaasiri baada ya safari ya karibu kilomita 300. Mwili utahifadhiwa kwenye Jumba la Holyroodhouse, makazi ya kifalme ya Scotland.

Mamia ya watu walijipanga barabarani huku gari la kubebea maiti lililobeba jeneza la Malkia Elizabeth wa Uingereza likipita katika kijiji cha Ballater, karibu na Balmoral, Scotland.

Umati wa watu ulitakiwa usirushe maua wakati msafara huo ukipita, ili usisumbue mpangilio sahihi wa safari ya mwisho ya mfalme huyo mwenye umri wa miaka 96, anayependwa sana nchini Uingereza.

Viongozi kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo akiwemo Rais wa Marekani Joe Biden, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese, pamoja na viongozi wengi.

Makumi ya maelfu ya watu wanapaswa pia kutoa heshima zao za mwisho kwake katika Ikulu ya Westminster, ambapo jeneza lake litawasili kuanzia Septemba 14 hadi 19, kabla ya kuhamishiwa huko Abbey, ambapo mazishi yatafanyika.

Mfalme Charles III alitawazwa kuwa mfalme siku ya Jumamosi katika sherehe za kuadhimisha miaka mia moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.