Pata taarifa kuu

Waingereza wagawanyika kuhusiana na gharama ya mazishi ya Elizabeth II

Wakati jeneza la Malkia Elizabeth II limewasili London, wapinzani wa utawala wa kifalme nchini Uingereza, karibu 20% ya raia kulingana na uchunguzi wa hivi karibuni, wanalaani fahari na gharama ya mazishi haya, ambayo ni zaidi ya kupita kiasi wakibaini kwamba nchi inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi.

Jeneza la Malkia Elizabeth II likiwa njiani kuelekea Kasri la Buckingham, London, Septemba 13, 2022.
Jeneza la Malkia Elizabeth II likiwa njiani kuelekea Kasri la Buckingham, London, Septemba 13, 2022. AFP - LOIC VENANCE
Matangazo ya kibiashara

 

Maombolezo na kutoa heshima vinaendelea nchini Uingereza baada ya kifo cha Elizabeth II Lakini kwa baadhi, sherehe zinazoandaliwa ni ghali sana nchini Uingereza, ambayo kwa sasa inapitia mgogoro mkubwa wa kiuchumi.

Kwa hivyo baadhi wameamua kususia mazishi ya malkia, hata kwenye Televisheni. Mmoja kati ya wapinzani wa utawala wa kifalme, Robert, mkazi wa moja ya vitongoji vya London, anaona ukubwa wa sherehe hizo ni wa kupita kiasi katika muktadha huu wa kiuchumi: “Kwa hakika inasikitisha sana kuona haya yote wakati watu watakuwa katika matatizo makubwa ya kulipa bili zao, kwa hakika tayari wameanza kuyaona! Hatuhitaji fahari hii yote, gharama zote hizi, safari hizi za kifalme kote nchini. Kitu cha kawaida zaidi kingetosha, kwa mfano katika ufalme wa Skandinavia au Uholanzi”.

"Ufalme ni mzuri kwa biashara"

Mazishi haya tayari yanafanyika kuwa ghali zaidi katika historia. Lakini hakuna kitu cha kashfa, amebaini Mark, mkazi mwingine wa mji wa London. "Ndio, inagharimu pesa, familia ya kifalme inagharimu pesa nyingi! Lakini hiyo sio sababu. Unapofikiria kila kitu ambacho ufalme umetupa, malkia hasa… Nadhani sio ghali sana, "anasema.

Madai wanayoyatoa mara kwa mara wafuasi wa ufalme: familia ya kifalme inagharimu pesa - euro milioni 50 kwa mwaka - lakini inaleta zaidi nchini kupitia utalii, lakini sio tu haya, anaelezea Andy, mjasiriamali ambaye anajionyesha kama mjasiriamali mwenye msimamo wa wastani. "Utawala wa kifalme si wa utalii pekee, pia ni mzuri kwa biashara,” amesema.

Waingereza wanakubaliana kwa hali yoyote juu ya hatua moja, mfalme mpya atalazimika kupunguza mtindo wa maisha wa familia ya kifalme. Lakini hiyo itakuwa baada ya mazishi yaliyopangwa kufanyika Septemba 19.

Mnamo Agosti, mfumuko wa bei ulifikia 10% nchini Uingereza, ambayo haijasikika kwa miaka arobaini. Na kuhusu bei ya nishati, imeongezeka kwa karibu 300% ikilinganishwa na mwezi Oktoba 2021. Kupanda kwa gharama ya maisha kumesababisha maelfu ya Waingereza kujiunga katika vuguvu linaloitwa "Don't pay" na kutishia kutolipa bili zao za umeme zinazofuata.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.