Pata taarifa kuu

Charles III atangazwa rasmi kuwa Mfalme wa Uingereza

Siku mbili baada ya kifo cha Malkia Elizabeth II, Charles III ametangazwa rasmi kuwa mfalme wa Uingereza Jumamosi hii. Charles III ametangazwa rasmi kama mfalme katika hafla ya kihistoria katika kasri la St James Jumamosi asubuhi.

Mfalme Charles III ametangazwa kuwa Mfalme wa Uingereza Jumamosi Septemba 10, 2022 huko London, Uingereza.
Mfalme Charles III ametangazwa kuwa Mfalme wa Uingereza Jumamosi Septemba 10, 2022 huko London, Uingereza. AP - Alberto Pezzali
Matangazo ya kibiashara

Ni mchakato ulioratibiwa ambao unapaswa kupelekea Charles III kutangazwa kama mfalme wa Uingereza. Baraza la kumtangaza rasmi mfalme huleta pamoja washiriki wa familia ya kifalme, wanasiasa, watu wa kidini na washauri wa kibinafsi wa Malkia. Baraza hilo limekutana katika Jumba la Mtakatifu James, karibu na Kasri la Buckingham huko London, kutangaza rasmi kifo cha Malkia Elizabeth II na kutangaza jina la mrithi wake.

Hii ni hatua muhimu kabla ya kutawazwa, mchakato ambao utafanyika baada ya miezi michache.

Siku ya Ijumaa, kutoka Buckingham Palace, Charles III alitoa hotuba yake ya kwanza ya televisheni kama mfalme, hotuba iliyorekodiwa ambapo alitoa heshima kubwa kwa "mama yake mpendwa".  Pia aliahidi kulitumikia taifa kwa uwajibikaji usiotetereka kama aliokuwa nao mamake Malkia katika utawala wake wa miaka 70..

Charles alipokea Ufalme punde tu baada ya kifo cha mamake Malkia Elizabeth II, lakini kikao rasmi cha kihistoria kilithibitisha jukumu lake Jumamosi. Baraza la kumtangaza rasmi Mfalme, linajumuisha wanasiasa wakuu, majaji na maafisa wengine walimtangaza rasmi kama mfalme. Ni mara ya kwanza hafla hii inapeperushwa kwenye televisheni.

Charles wa III alichukua mikoba ya Ufalme moja kwa moja mara baada ya kifo cha mama yake Malkia Elizabeth wa Pili kilichotokea siku ya Alhamis, lakini sherehe za kutawazwa ni hatua muhimu ya kikatiba ya kumtambulisha Mfalme mpya nchini humo.

Hii ni mara ya kwanza kwa hafla hiyo kufanyika tangu mwaka 1952 wakati Elizabeth alipotawazwa rasmi kuwa Malkia. Mfalme Charles wa III ameahidi kufuata nyayo za mama yake wakati wa hotuba yake ya kwanza aliyoitoa hapa jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.