Pata taarifa kuu

Wakenya wanatarajia msamaha na fidia kutoka kwa mtawala mpya Charles III

Nchini Kenya, utawala wa Malkia wa Uingereza hauachi tu kumbukumbu chanya. Ukoloni wa Uingereza uliacha makovu na wengi bado wanasubiri msamaha na fidia kwa ukatili uliofanywa wakati wa ukoloni. Faili inayomngoja Mfalme Charles III wakati London haijaomba msamaha hadi leo.

Mfanyabiashara anayeuza magazeti ya kila siku ambavyo vimechapisha habari kuhusu kifo cha Malkia Elizabeth II, Nairobi mnamo Septemba 09, 2022.
Mfanyabiashara anayeuza magazeti ya kila siku ambavyo vimechapisha habari kuhusu kifo cha Malkia Elizabeth II, Nairobi mnamo Septemba 09, 2022. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Kenya imekuwa na uhusiano wa kipekee na Elizabeth II tangu Februari 6, 1952 wakati, alipokuwa ziarani nchini humo, alipata taarifa kuhusu kifo cha baba yake na hivyo kuwa Malkia wa Uingereza.

Lakini wakati huu pia unaambatana na mwanzo wa uasi wa Mau Mau, waasi waliokuwa wakipinga ukoloni. Kipindi ambacho London ilionyesha masikitiko yake mwaka wa 2013 kwa baadhi ya visa vya unyanyasaji uliofanywa wakati wa ukandamizaji wa Uingereza dhidi ya waasi wa Mau Mau katika miaka ya 1950. London ilikuwa imewafidia zaidi ya maveterani 5,000.

Lakini waathiriwa wengine wengi bado wanangojea kufidiwa. Jamii za Kipsigis na Talai, wanataka kulipwa fidia kwa kudhulumiwa na kufukuzwa kutoka kwa mashamba yao kwa manufaa ya mashamba ya chai, huko Kericho, magharibi mwa Kenya. Malalamiko ambaypo pia yaliwasilishwa mwezi Agosti mbele ya Mahakama ya Haki ya Ulaya. "Majibu ya serikali ya Uingereza hayajawahi kuridhisha," amesema Joel Kimutai Bosek, mmoja wa mawakili wanaowakilisha waathiriwa 150,000.

"Haya ni makovu ya kutisha ya Jumuiya ya Madola"

Waingereza "wamechukua mtazamo wa 'Sijali', wakipuuza madai ya fidia badala ya kuwajibika kwa matendo yao", amesema wakili huyo. Lakini bado ana matumaini: "Tunaweza tu kutumaini kwamba Charles atakuwa na mtazamo tofauti. Anapaswa kutambua kwamba familia yake haikuwa na jukumu chanya tu. Iwapo ataendelea kushikilia Jumuiya ya Madola pamoja, ni lazima ahakikishe kwamba dhuluma zilizopita zinatatuliwa. Haya ni makovu ya kutisha ya Jumuiya ya Madola”.

Wakati huo huo, ardhi hizi bado zinatumika leo kwa kilimo cha chai inayouzwa nje na mashirika makubwa ya kimataifa. Mnamo mwezi Mei, wawakilishi wa waathiriwa walimwandikia barua Prince William lakini barua hiyo haikujibiwa. Muda unakwenda, anasisitiza Joel Kimutai Bosek, kwa sababu wengi wa waathiriwa tayari ni wazee.

Kufuatia kutangazwa kwa kifo cha Malkia, Rais anayemaliza muda wake, Uhuru Kenyatta alitangaza kipindi cha maombolezo ya kitaifa nchini Kenya. Katika kumuenzi marehemu, bendera za Kenya zitapandishwa nusu mlingoti katika ofisi za serikali hadi Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.