Pata taarifa kuu

Malkia Elizabeth II afariki dunia akiwa na miaka 96

Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, kiongozi aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi duniani kwa miaka 70, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96.

Malkia Elizabeth wa II, wa Uingereza. 24/06/2015.
Malkia Elizabeth wa II, wa Uingereza. 24/06/2015. AP - Markus Schreiber
Matangazo ya kibiashara

Familia yake ilikusanyika katika makazi yake ya Scottish, baada ya taarifa kuwa madaktari wake walikuwa wamemuweka chini ya uangalizi maalumu.

Malkia Elizabeth II, aliingia madarakani mwaka 1952 ambapo katika kipindi chake alishuhudia mabadiliko mbalimbali.

Kufuatia kifo chake, mtoto wake mkubwa Charles, mwanamfalme wa zamani wa Wales, ataiongoza nchi hiyo katika kipindi hiki cha maombolezo kama Mfalme mpya na kiongozi wa serikali.

Katika taarifa yake, kasri la Buckingham limesema "Malkia alifariki akiwa mtulivu katika makazi yake ya Balmoral, mchana wa leo.

"Mfalme na malkia watabaki balmoral jioni hii na watarejea London, kesho asubuhi."

Watoto wa malkia walisafiri kuelekea Balmoral, jirani na mji wa Aberg-deen, baada ya madaktari kumueweka malkia Elizabeth II katika uangalizi wa karibu.

Wajukuu zake, mwanamfalme William, pia yuko huko, pamoja na mdogo wake, mwanamfalme Henry pia nae ameelekea huko.

Utawala wa Malkia Elizabeth II kama kiongozi wa nchi, ulianzia na hata kushuhudia mabadiliko baada ya vita ya dunia hadi kuwa malkia wa Jumuiya ya madola, kumalizika kwa vita baridi na pia kushuhudia nchi yake ikiingia kuwa mwanachama wa umoja wa Ulaya na hadi ilipojitoa.

Utawala wake umeshuhudia kupita kwa mawaziri wakuu 15, kuanzia kwa Wiston Churchill, aliyezaliwa 1874, na sasa Liz Truss aliyezaliwa miaka 101 baadae mwaka 1975, na alichaguliwa na malkia wiki hii.

Amekuwa akiongoza vikao na mawaziri wakuu wote kila wiki.

Katika kasri la Buckingham, raia wamekusanyika kusubiri taarifa zaidi kuhusu malkia kabla ya baadae wengi kuonekana wakiangua kilio baada ya kupata taarifa za kifo chake.

Bendera zote nchinik humo sasa zinapeperushwa nusu mlingoti.

Malkia alizaliwa na Elizabeth Alexandra Mary Windsor, katika kitongoji cha Mayfair, jijinik London, tarehe 21 April mwaka 1926.

Wachache hawakuamini kama angeweza kuja kuwa malkia wa Uingereza, lakinik mwezi Desmemba mwaka 1936 mjomba wake, Edward VIII, alijiuzuru kwenye nafasi yake baada ya kumuoa mwanamke wa kimarekani aliyeachika mara mbili, Wallis Simpson.

Baba yake Elizabeth, King Geaorge VI akateuliwa kuwa mfalme wa nchi hiyo.

Ndani ya miaka mitatu, Uingereza iliingia vitani dhidi ya utawala wa kinazi wa Kijerumani, Elizabeth na mdogo wake Margareth, walitumia muda mwingi katika kasri, baada ya wazazi wao kukataa wahamishiwe Canada.

Baada ya kufikisha miaka 18, Elizabeth alitumia karibuj miezi 5 chini ya uangalizi ambapo alijifunza masuala kadhaa ikiwemo ufundi na kuendesha magari.

Katika kipindi chote cha vita, Elizabeth alikuwa akitumiana barua na binamu yake Philip, mwanamfalme wa Ugiriki, ambaye alikuwa akihudumu katika jeshi la wanamaji.

Mapenzi yao yaliimarika na baadae walioana tarehe 20 Novemba mwaka 1947, mwanamfalme akichukua jina la Duke of Edinburgh, kabla ya kufariki mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 99.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.