Pata taarifa kuu

Viongozi mbalimbali duniani watoa rambirambi kwa familia ya Malkia Elizabeth II

Viongozi wa dunia wameendelea kutuma risala za rambirambi na kumkubuka Malkia wa Uingereza Elizabeth II, aliyefariki jana akiwa na uamuri wa miaka 96, akiwa nyumbani kwake huko Scotland. 

Mtu huyu akitazama picha za Malkia Elizabeth wa Pili kwenye dirisha karibu na Windsor Castle, Ijumaa, Septemba 9, 2022. Malkia Elizabeth II, kiongozi aliyetawala kwa muda mrefu zaidi nchini Uingereza, alifariki Alhamisi baada ya miaka 70 kwenye uongozi wa nchi. Alikuwa na umri wa miaka 96.
Mtu huyu akitazama picha za Malkia Elizabeth wa Pili kwenye dirisha karibu na Windsor Castle, Ijumaa, Septemba 9, 2022. Malkia Elizabeth II, kiongozi aliyetawala kwa muda mrefu zaidi nchini Uingereza, alifariki Alhamisi baada ya miaka 70 kwenye uongozi wa nchi. Alikuwa na umri wa miaka 96. © AP Photo/Frank Augstein
Matangazo ya kibiashara

Salamu hizo zimetoka katika kona zote za dunia, zikiwemo zile alizoongoza kipindi cha ukoloni lakini pia kutoka kwa viongozi wa mataifa 14 kwenye Jumuiya ya nchi za Madola ambayo amekuwa kiongozi tangu alipokuwa Malkia mwaka 1952. 

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ameemwelezea Malkia Elizabeth wa pili kama kiongozi aliyekuwa rafiki wa Ufaransa na aliyeacha alama kwa nchi yake. 

Rais wa Marekani Joe Biden, amwelezea kama kiongozi ambaye maadili yake hayawezi kulinganishwa na kuagiza bendera kupepea nusu mlingoti katika Ikulu ya White House na majengo ya serikali, katika kipindi cha maambolezo. 

Viongozi wengine wa dunia waliomkumbuka Malkia Elizabeth wa pili, ni pamoja na rais Urusi Vladimir Putin ambaye ametoa salamu za pole kwa família yake, sawa na rais Xi Jinping wa China. 

Viongozi wa mataifa ya Afrika pia, hawajaachwa nyuma, rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema maisha ya Malkia Elizabeth yamemkumbusha yale ya Nelson Mandela, huku rais wa Kenya anayeondoka madarakani Uhuru Kenyatta akimwelezea kama nyota aliyejotolea kwa utumishi wa watu. 

Naye kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amesema amesikitishwa na kifo cha Malkia na kumkumbuka kama kiongozi aliyehimiza maridhiano. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.