Pata taarifa kuu

Kifo cha Elizabeth II: Mizinga 96 yafyatuliwa kote Uingereza kama kumuaga Malkia

Mizinga imesikika kote Uingereza siku ya Ijumaa. Saa nane mchana (saa za Ufaransa), saa moja baada ya kusalia kimya kwa dakika moja kwa kutoa heshima kwa Malkia Elizabeth II baada ya kuiaga dunia na kumalizika kwa utawala wake kama malkia, mizinga 96 imepigwa kwa kutoa heshima kwa kiongozi huyo.

Mfalme wa Uingereza Charles III na Malkia Consort Camila wanawasili katika Kasri la Buckingham, ambapo kumekuwa kukitolewa heshima kwa Elizabeth II, huko London mnamo Septemba 9, 2022.
Mfalme wa Uingereza Charles III na Malkia Consort Camila wanawasili katika Kasri la Buckingham, ambapo kumekuwa kukitolewa heshima kwa Elizabeth II, huko London mnamo Septemba 9, 2022. Β© Yui Mok / AP
Matangazo ya kibiashara

Mizinga imepigwa katika miji mbalimbali kama London, Hyde Park na kwenye minara ya mji wa London. Miji mingine nchini Uingereza kama vile York, Colchester, lakini pia Belfast katika Ireland ya Kaskazini, Cardiff katika Wales au Edinburgh katika Scotland pia mizinga ilisikika.Β 

Mizinga ilifyatuliwa pia kwenye kambi za vikosi vya majini, kwenye eneo la kiakiolojia ya Stonehenge au eneo la Gibraltar kwenye rasi ya Iberia.

Kila mzinga unawakilisha mwaka mmoja ya maisha ya Elizabeth II, ambaye aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 96. Baada ya kutawazwa kwake kwenye kiti cha enzi akiwa na umri wa miaka 27, utawala wake ulidumu miaka 70, mojawapo ya tawala uliodumu kipindi kirefu zaidi katika historia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.