Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Malkia Elizabeth wa pili, kutohudhuria ibada ya kushukuru

Malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili, anayeadhimisha miaka 70 katika nafasi hiyo, hatahudhuria ibada ya kitaifa katika Kanisa la Mtakatifu Paulo jijini London Siku ya Ijumaa , kufuatia kile kinachoelezwa kutojisikia vema kimwili.

Malkia Elizabeth wa pili  Elizabeth, (Kushoto) akiwa na familia yake katika jengo la Kasri yake jijini London Juni 2 2022
Malkia Elizabeth wa pili Elizabeth, (Kushoto) akiwa na familia yake katika jengo la Kasri yake jijini London Juni 2 2022 REUTERS - HANNAH MCKAY
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya kushuhudia Gwaride na shamrashamra za kijeshi kutokea kwenye eneo la Kasri yake siku ya Alhamisi akiwa, akiwa na familia yake.

Aidha, imeelezwa kuwa uamuzi wa Malkia huyo mwenye umri wa miaka 96, kutohudhuria ibada hiyo, umefanywa kwa kusitasita kwa kuzingatia mwendo wa kuelekea Kanisani, na shughuli zitakazofuata.

Hata hivyo, siku ya Alhamisi, alishiriki kwenye hafla ya kuwasha taa.

Maadhimisho haya ya miaka sabini, yanaelezwa kuwa ya kipekee na wachambizi wa mambo wanaona huenda kusitokee kiongozi mwingine atakayekaa madarakani kwa kipindi hicho chote.

Malkia Elizabeth wa polisi, aliingia katika nafasi hiyo Juni, 2 mwaka 1953, akiwa na umri wa miaka 25, baada ya baba yake George V1 kufariki dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.