Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Australia: Watu sita wauawa kwa shambulio la kisu Sydney

Watu sita wameuawa katika shambulio la kisu siku ya Jumamosi Aprili 13 katika kituo cha biashara huko Sydney, nchini Australia. Mshambulaji ambaye nia yake haijajulikana kwa sasa, aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Maafisa wa idara ya huduma za dharura karibu na Bondi Junction baada ya watu kadhaa kudungwa kisu ndani ya jumba la biasha la Westfield Bondi Junction huko Sydney, Aprili 13, 2024.
Maafisa wa idara ya huduma za dharura karibu na Bondi Junction baada ya watu kadhaa kudungwa kisu ndani ya jumba la biasha la Westfield Bondi Junction huko Sydney, Aprili 13, 2024. via REUTERS - AAP
Matangazo ya kibiashara

Mhusika wa shambulio hilo anaonekana "alitenda peke yake", Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese almesema katika mkutano na waandishi wa habari. "Kwetu sote jioni hii, matukio ya kuogofya ya Bondi Junction hayaelezeki na hayaeleweki," amesema pia.

Shambulio hili nchini Australia pia limejeruhi watu kadhaa. Hali ya watu kadhaa waliokimbizwa hospitali bado haijafahamika, akiwemo mtoto wa miezi tisa.

Mshambuliaji aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi mwanamke, mmoja wa watu wa kwanza kufika eneo la tukio, wakati akielekea kwake, kisu kikielekeza upande wake. Sababu ya shambulio hili bado haijajulikana. Polisi pia wanaonyesha kwamba kwa kuzingatia ushahidi wa kwanza uliokusanywa, hakuna kitu kinachoonyesha kwamba mshambuliaji alichochewa na itikadi fulani.

Mkasa huo ulitokea katika jumba kubwa la biashara la Westfield Bondi Junction, ambalo lilikuwa limejaa wanunuzi Jumamosi alasiri. Walioshuhudia wameeleza matukio ya hofu, huku wateja wakikimbia kutafuta hifadhi na polisi wakijaribu kulinda eneo hilo.

Mwanaume mwenye kisu kikubwa mkononi

Picha za kamera za usalama zinazorushwa na vyombo vya habari nchini humo zinaonyesha mwanamume mmoja akikimbia kwenye jumba hilo akiwa na kisu kikubwa mkononi na kuwajeruhi watu wakiwa wamelala chini. Tukio la aina hii, ambalo ni nadra sana nchini Australia, limeifanya nchi hiyo kustaajabishwa, anaripoti mwandishi wetu katika Sydney, Grégory Plesse.

"Mawazo ya kwanza ya Waaustralia wote ni kwa wale walioathiriwa na kwa wapendwa wao," Waziri Mkuu Anthony Albanese ameandika kwenye mtandao wa kijamii.

  Mfalme Charles III, kiongozi wa Uingereza, lakini pia mkuu wa serikali ya Australia, amesema "kuhuzunishwa" katika taarifa yake. Charles III anaongeza kuwa "mawazo yake yako kwa familia na wapendwa wa wale waliouawa kikatili katika shambulio hili lisilo na maana".

Kwa upande wake, "Papa Francis alihuzunishwa sana kuhusu shambulio la kikatili huko Sydney, na kuwasilisha mshikamano wake wa kiroho kwa wale wote walioathiriwa na janga hili lisilo na maana," amebinisha Pietro Parolin, nambari mbili wa Vatican, katibu kiongozi , katika telegramu kwa Askofu Mkuu wa Sydney Anthony Colin Fisher.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.