Pata taarifa kuu

Australia kuimarisha zaidi jeshi lake la wanamaji

Serikali ya Australia inapanga kuongeza maradufu idadi ya meli zake kubwa za kivita. Imewasilisha mpango siku ya Jumanne wa kuongeza matumizi ya ulinzi hadi 2.4% ya pato la taifa (GDP), zaidi ya lengo la 2% lililowekwa na washirika wake wa NATO. Imekusudiwa kuhakikisha usalama wa njia za baharini. Tangazo hilo linakuja baada ya ongezeko kubwa la moto kutoka China na Urusi katika eneo hilo.

Canberra inapanga kuongeza matumizi yake ya ulinzi kwa zaidi ya Euro bilioni 6.5, ikilenga meli kubwa 26 katika muongo ujao, zaidi ya mara mbili ya meli 11 ilizo nazo sasa.
Canberra inapanga kuongeza matumizi yake ya ulinzi kwa zaidi ya Euro bilioni 6.5, ikilenga meli kubwa 26 katika muongo ujao, zaidi ya mara mbili ya meli 11 ilizo nazo sasa. © Petty Officer 3rd Class Isaak Martinez/Australian Defense Force via AP
Matangazo ya kibiashara

Mbio za kupata silaha zinaendelea katika eneo la Asia-Pacific. Siku ya Jumanne Februari 20, Australia imewasilisha mpango wa kuimarisha jeshi lake la wanamaji, kwa kuongeza maradufu idadi ya meli zake kubwa za kivita, ikilenga kiwango ambacho hakijawahi kutokea tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Canberra inapanga kuongeza matumizi yake ya ulinzi kwa zaidi ya Euro bilioni 6.5, ikilenga meli kubwa 26 katika muongo ujao, zaidi ya mara mbili ya meli 11 ilizo nazo sasa.

"Hiki ndicho kikosi kikubwa zaidi tutakuwa nacho tangu mwisho wa Vita vya Pili vya Dunia," Waziri wa Ulinzi wa Australia Richard Marles amesema.

"Jeshi la Kifalme la Australia lazima liwe na uwezo wa kuhakikisha usalama na usalama wa njia zetu za meli (...) kwa kuwa ni muhimu kwa njia yetu ya maisha na ustawi," ameongeza.

Australia itaongeza meli kubwa sita za daraja la Hunter, meli tatu kubwa maalumu za kivita, meli 11 za majukumu mbalimbali na meli zingine sita za kivita za hali ya juu zenye uwezo wa kufanya kazi bila rubani.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.