Pata taarifa kuu

Australia: Kimbunga chaua watu tisa kwenye Pwani ya Mashariki

Kimbunga kimeua watu tisa kwenye pwani ya mashariki ya Australia, mamlaka imetangaza leo Jumatano, eneo ambalo zaidi ya nyumba 80,000 zimesalia bila umeme.

Operesheni ya uokoaji baada ya mvua kubwa kunyesha huko Gippsland, kaskazini mashariki mwa Melbourne, katika jimbo la Victoria la Australia, Desemba 27, 2023.
Operesheni ya uokoaji baada ya mvua kubwa kunyesha huko Gippsland, kaskazini mashariki mwa Melbourne, katika jimbo la Victoria la Australia, Desemba 27, 2023. © AFP PHOTO / VICTORIA POLICE
Matangazo ya kibiashara

Wahanga waliofariki, akiwemo msichana wa umri wa miaka tisa, walikuwa katika majimbo ya Queensland na Victoria, yaliyokumbwa na radi na upepo mkali tangu Jumatatu, na kusababisha kuanguka kwa miti na mafuriko.

Boti iliyokuwa na watu kumi na moja ilipinduka karibu na Brisbane, na kusababisha vifo vya wanaume watatu kwa kuzama, imesema polisi, ambayo imepata maiti ya tatusiku ya Jumatano.

Wafanyakazi wengine wanane iongoni mwa wafanyakazi wa boti hili, ambao walikuwa katikati ya safari ya uvuvi, walisafirishwa hadi hospitali.

"Saa 24 zilizopita zimekuwa mbaya kutokana na hali ya hewa," Mkuu wa Polisi wa Queensland Katarina Carroll amewaambia waandishi wa habari.

Huko Gympie (mashariki), wanawake wawili waliuawa baada ya kudondoka kwenye shimo kubwa la maji ya mvua, na mwanamke wa tatu, ambaye alinusurika, vikosi vya polisi vimesema.

Eneo la Queensland bado liko katika hatari ya mvua za radi "hatari", mafuriko "yanayoweza kutishia maisha", ,mamlaka ya Hali ya Hewa ya Australia imeonya.

Zaidi ya nyumba 80,000 zimesalia bila umeme, limesema shirika la umeme la Energex, ambaylo Jumanne lilisikitishwa na zaidi ya wateja 120,000 walioathiriwa na kukatika kwa umeme.

"Kimbunga kilikuwa na nguvu kiasi gani? Nguvu ya kutosha kuharibu nguzo kadhaa zilizojengwa kwa saruji zinazoshikilia waya zonazosafirisha umeme wenye nguvu kubwa," shirika la umeme limesema kwenye mitandao ya kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.