Pata taarifa kuu

EU yafungua mlango wake kwa Ukraine, lakini yashindwa kuthibitisha msaada mpya

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameshindwa usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa kuishawishi Hungary kuondoa kura yake ya turufu juu ya msaada mpya wa euro bilioni 50 kwa Ukraine, baada ya kufanikiwa mapema kufungua mazungumzo ya kujiunga na nchi hii iliyo katika vita.

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, mbele kulia, akizungumza na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, mbele wa pili kulia, na Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban, katikati ya mstari wa pili, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya. Brussels mnamo Alhamisi, Feb. 9, 2023. Umoja wa Ulaya uliamua Alhamisi, Desemba 14, 2023 kufungua mazungumzo ya kujiunga na Ukraine, jambo ambalo lilikuwa ni badiliko la kushangaza kwa nchi iliyo kwenye vita ambayo ilikuwa imetatizika kupata uungwaji mkono unaohitajika kwa matakwa yake ya uanachama na kukabiliwa na upinzani wa muda mrefu kutoka kwa Waziri Mkuu wa Hungary Victor Orban.
Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, mbele kulia, akizungumza na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, mbele wa pili kulia, na Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban, katikati ya mstari wa pili, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya. Brussels mnamo Alhamisi, Feb. 9, 2023. Umoja wa Ulaya uliamua Alhamisi, Desemba 14, 2023 kufungua mazungumzo ya kujiunga na Ukraine, jambo ambalo lilikuwa ni badiliko la kushangaza kwa nchi iliyo kwenye vita ambayo ilikuwa imetatizika kupata uungwaji mkono unaohitajika kwa matakwa yake ya uanachama na kukabiliwa na upinzani wa muda mrefu kutoka kwa Waziri Mkuu wa Hungary Victor Orban. AP - Virginia Mayo
Matangazo ya kibiashara

"Muhtasari wa usiku: kura ya turufu kwa fedha za ziada kwa Ukraine" kama kwa mapendekezo ya marekebisho ya bajeti ya Ulaya, Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban amesema kwenye X (zamani ikiitwa Twitter).

Mataifa mengine 26 ya Umoja wa Ulaya, yalikutana na Hungary katika mkutano wa kilele mjini Brussels, ilibidi wakubali msimamo wa kiongozi wa Hungary.

"Tutarejea kwenye suala hili mwanzoni mwa mwezi wa Januari" wakati wa mkutano mwingine, amesema Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel katikati ya usiku.

"Kuna nchi 26 ambazo zimeidhinisha msaada huu. Hakuna makubaliano na Hungary kwa sasa, lakini nina imani kuwa tutayafanikisha mwaka ujao," ameongeza Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte.

EU ilikuwa imepanga kuipatia Ukraine msaada wa euro bilioni 50, mikopo ya bilioni 33 na ruzuku ya euro bilioni 17, katika kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka ujao.

Msaada huu mpya unachukuliwa kuwa muhimu katika Kyiv wakati msaada wa Marekani wa zaidi ya dola bilioni 60 bado umezuiwa katika Bunge la Congress kutokana na kusita kwa wabunge wa chama cha Republican.

Kiongozi wa Hungary hakushiriki kura

Hata hivyo, viongozi wa Ulaya walikuwa wameweza saa chache mapema kukubaliana juu ya kufunguliwa kwa mazungumzo ya kujiunga na Ukraine.

Bw. Orban wakati huo alikubali kujizuia, ili asilazimike kuidhinisha uamuzi ambao ameendelea kuuona kuwa mbaya kwa mustakabali wa Umoja wa Ulaya.

Kiongozi wa Hungary "hakuwa ukumbini wakati azimio hilo lilipopitishwa, alikubali kufanya hivyo", mwanadiplomasia wa Ulaya ambaye aliomba kutotajwa jina jina ameliambia shirka la habari la AFP. "Ni suluhisho la kisayansi (...) Ishara ya kisiasa imetolewa," ameongeza.

Katika video iliyochapishwa kwenye Facebook, Viktor Orban kisha alieleza kwamba nchi yake haikutaka "kushiriki jukumu" la uchaguzi huu "usio na maana" wa nchi zingine 26 na kwa hivyo "alijizuia".

"Ni ushindi kwa Ukraine, kwa Ulaya yote, ushindi unaotia motisha, hututia moyo na kutufanya tuwe na nguvu zaidi", alisema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, huku Ikulu ya Marekani ikikaribisha "uamuzi wa kihistoria" .

Ingawa mchakato utakuwa mrefu, ishara ni kubwa kwa nchi hii iliyo kwenye vita tangu Februari 24, 2022, tarehe ya kuanza kwa uvamizi wa Urusi.

Charles Michel amesema uamuzi huu wa kufungua mazungumzo na Ukraine, lakini pia na Moldova, ni "ishara ya wazi ya matumaini kwa raia wa nchi hizi na kwa bara letu".

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alikaribisha "ishara kali ya uungaji mkono" kwa Ukraine ambayo inatoa "mtazamo" kwa nchi hii. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alizungumzia "jibu la kimantiki, la haki na la lazima" kwa matarajio ya watu wake.

- Ishara ya kutia moyo -

Saa chache mapema, Bw. Orban hata hivyo alisisitiza kukataa kwake kukubali hatua hii. "Hakuna sababu ya kujadili chochote, kwa sababu masharti hayajatimizwa," alisema kwa ugomvi mwanzoni mwa mkutano huo.

Volodymyr Zelensky alikuwa akingojea, kama mamilioni ya Waukraine, ishara ya kutiwa moyo na Wazungu, wakati ambapo ishara hasi kutoka Washington zinaongezeka.

Kwa wiki kadhaa, mawingu yamekuwa yakitanda Ukraine: mashambulizi yake ya kijeshi hayajaleta mafanikio makubwa na misaada ya Magharibi, muhimu kwa juhudi za vita, imezuiwa.

Wakati huo huo wakati mkutano muhimu wa kilele huko Brussels ulianza, Vladimir Putin, kwa kulinganisha, alionyesha imani yake katika ushindi kwa Moscow. "Kwa kweli katika urefu wote wa laini ya mawasiliano, vikosi vyetu vya jeshi vinaboresha ngome zao," rais wa Urusi alisema.

"Ikiwa Putin atashinda Ukraine, kuna hatari kubwa kwamba uchokozi wake hautaishia hapo," alionya Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, kwa pamoja na viongozi kadhaa wa Ulaya.

EU pia iliamua kutoa hadhi ya nchi ya mgombea kwa Georgia na kufungua, chini ya masharti, mazungumzo ya kujiunga na Bosnia-Herzegovina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.