Pata taarifa kuu

Viktor Orban: EU bado haiwezi kujadili uanachama wa Ukraine

Waziri Mkuu w Hungary, Viktor Orban, ametishia kuzuia mpango wa Umoja wa Ulaya, kuongeza msaada kwa Ukraine na kuharakisha mchakato wa kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya. 

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ahudhuria mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya, mjini Brussels, Ubelgiji Desemba 14, 2023.
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ahudhuria mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya, mjini Brussels, Ubelgiji Desemba 14, 2023. REUTERS - YVES HERMAN
Matangazo ya kibiashara

Orban ametoa kauli hiyo jijini Brussels, wanakokutana wakuu wa nchi za EU, kujadili mpango wa kuipa Ukraine Euro Bilioni 50 kwa kipindi cha miaka minne ijayo. 

 Naye rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky akiwahotubia viongozi hao kwa njia ya video, amewataka kuharakisha mchakato wa nchi yake kuwa mwanachama wa EU ili kuinyima Urusi ushindi wa kisiasa. 

 Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano wake wa kwanza wa mwisho wa mwaka na wanahabari,  amesema, malengo ya nchi yake nchini Ukraine, hayajabadilika, na hakutakuwa na amani hadi pale yatakapotimia. 

 Putin ametoa kauli hii, siku chache baada ya kutangaza kuwania tena urais mwezi Machi. Huo utakuwa muhula wake wa tano kwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 71, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 24.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.