Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen yuko nchini Ukraine
Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amewasili mjini Kyiv kujadiliana na rais Volodymr Zelensky kuhusu mchakato wa nchi yake kujiunga katika Umoja wa Ulaya.
Imechapishwa:
Kyiv iliwasilisha maombi ya kupewa uanachama wa EU siku chache tu baada ya uvamizi wa Urusi mnamo Februari 24, 2022.
Kupitia ukurasa wake wa X, zamani ukiitwa Twitter, kiongozi huyo ameongeza kuwa watajadili suala la msaada wa kifedha wa EU kujenga upya Ukraine kama demokrasia ya kisasa na yenye mafanikio.
Good to be back in Kyiv for my 6th war time visit.
— Ursula von der Leyen (@vonderleyen) November 4, 2023
I’m here to discuss Ukraine’s accession path to the EU.
The EU’s financial support to rebuild Ukraine as a modern, prosperous democracy.
And how we will continue to make Russia pay for its war of aggression. pic.twitter.com/dLJ6bUz4UU
Ziara ya Jumamosi ni ya sita kwa von der Leyen nchini Ukraine tangu vita kati yake na Urusi kuanza.
Ziara hiyo inakuja huku kukiwa na wasiwasi kwamba uungwaji mkono kwa Ukraine kutoka kwa washirika wake huenda ukapungua kutokana na mapigano yanayoendelea huko Mashariki ya kati.
Von der Leyen ameeleza kuwa safari yake ilikuwa imepangwa kwa muda mrefu na kwamba ilikuwa ni ziara ya kitamaduni kufanya kabla ya kuwasilisha ripoti kuhusu kupokea wanachama wapya wa EU.
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba aliwaambia waandishi wa habari wiki hii kwamba Kyiv iko mbioni kutimiza wajibu wake wa kufungua mazungumzo kuhusu uanachama wa Umoja wa Ulaya, na von der Leyen alikiri mwezi Septemba kwamba Kyiv imepiga hatua kubwa katika jitihada zake za kuwa mwanachama wa EU.