Pata taarifa kuu

Mawaziri wa mambo ya nje wa EU wanakutana nchini Ukraine

Nairobi – Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka mataifa ya Umoja wa Ulaya, wanakutana katika jiji kuu la Ukraine Kyiv kwa kongamano la kihistoria ambalo kwa mara kwanza linafanyika nje ya mipaka ya Umoja huo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky  ameendelea kushinika nchi yake kupewa uanachama wa Umoja wa Ulaya
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky  ameendelea kushinika nchi yake kupewa uanachama wa Umoja wa Ulaya AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unafanyika wakati huu Kyiv ikiendelea kutoa wito wa kujiunga na EU katika siku zijazo, wakati huu pia ikiendelea kupambana dhidi ya uvamizi wa Urusi ambao unaingia mwezi wa ishirini sasa.

Kwa mujibu wa waziri wa sera za kigeni katika umoja huo Josep Borrell, wamekutana jijini Kyiv, mwanachama ajaye wa Umoja huo kama njia moja ya kuonyesha mshikamano na Ukraine.

Aidha kiongozi huyo ameeleza kuwa hatima ya baadae ya Ukraine iko mikononi mwa Umoja wa Ulaya, Kyiv kwa upande wake ikipongeza hatua ya kuaandaliwa kwa mkutano huo katika ardhi yake.

Naye waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba, amewaambia wanahabari kwamba hatua hii ni ya kihistoria kwa taifa lake.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky  ameendelea kushinika nchi yake kupewa uanachama wa Umoja wa Ulaya kutokana na hatua ya Moscow kuivamia ardhi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.