Pata taarifa kuu

Migogoro inayoikabili EU katikati mwa hotuba ya Ursula von der Leyen kuhusu hali ya Umoja

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen anatarajiwa kutoa hotuba yake ya sera kwenye Bunge la Ulaya siku ya Jumatano. Inatarajiwa katika masuala mengi, kama vile mfumuko wa bei au mgogoro wa nishati. Ikiwa mwaka jana, Ursula von der Leyen aliweza kupongeza EU juu ya usimamizi wa janga la UVIKO au kuonyesha uthabiti juu ya sheria katika Ulaya ya Kati, hotuba ya mwaka huu inakuja wakati mzozo Umoja wa Ulaya unakabiliwa na migogoro mbalimbali.

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen.
Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen. AP - Virginia Mayo
Matangazo ya kibiashara

Kiini cha hotuba hii kuhusu hali ya Muungano ni vita dhidi ya bara la Ulaya, anaripoti mwandishi wetu mjini Brussels, Pierre Benazet. Kama vile Umoja wa Ulaya na taasisi zake ilikuwa kama mtazamaji wakati wa vita vya Yugoslavia miaka 30 iliyopita, na leo wanahusishwa katika mzozo wa Ukraine.

Wasiwasi kuu wa wakati huu ni dhahiri shida ya nishati ambayo inaendelea kuzigawanya serikali 27 za Muungano. Na hii ndiyo kesi hasa kuhusu kuanzishwa kwa bei ya chini ya gesi inayoagizwa kutoka Urusi, ambayo wengine kama Hungaria wanakataa huku wengine kama Ubelgiji wanataka kwenda mbali zaidi.

Kwa hivyo Tume italazimika kupendekeza masuluhisho ya kiubunifu ya nishati, kama Waziri Mkuu wa Ufini Sanna Marin alivyouliza Jumanne katika hotuba kwenye jukwaa hili la Bunge la Strasbourg. Sanna Marin alimwomba Rais wa Tume ya Ulaya "suluhisho mpya za ujasiri" ili kupunguza bei ya umeme inayolipwa na famili na makampuni. "Sasa tunalipa bei ya juu sana kwa utegemezi wetu kwa nishati ya Urusi. Bei na vita vya nishati pia inaleta tishio la mzozo wa chakula duniani,” alionya.

Suala la umoja wa Ulaya linapaswa pia kuwa kitovu cha hotuba ya Ursula von der Leyen, pamoja na mshikamano na, dhahiri katika mstari wa kuona, upunguzaji mzuri wa bei ya nishati, njia pekee ya kuwashawishi raia wa Ulaya kwamba kusaidia Ukraine kwa vita vyake dhidi ya Urusi havitaleta madhara yoyote kwa mustakabali wa kiuchumi wa Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.