Pata taarifa kuu

Gesi: Urusi na Gazprom zaweka shinikizo kwa mshikamano wa Ulaya kwa kufunga bomba

Kampuni ya Gesi ya Urusi, Gazprom, imetangaza mnamo Septemba 3 kwamba usambazaji wa gesi kwenda Ulaya utapitia bomba la Ukraine. 

Ofisi za kampuni kubwa ya gesi ya Gazprom huko Moscow mnamo Septemba 2021.
Ofisi za kampuni kubwa ya gesi ya Gazprom huko Moscow mnamo Septemba 2021. AFP - ALEXANDER NEMENOV
Matangazo ya kibiashara

Kampuni hiyo kubwa ya gesi ya Urusi ilieleza Ijumaa jioni kwamba bomba la gesi la Nord Stream 1 halitarejesha huduma kwa sababu ya hitilafu ya kiufundi. Mkakati wa kidiplomasia kusambaratisha mshikamano wa nchi za Ulaya, kulingana na Francis Perrin, mtaalamu wa hidrokaboni na mtafiti katika taasisi ya IRIS. Kwa upande wa Brussels, wanajaribu kuwahakikishia watumiaji wa bidhaa hiyo muhimu Ulaya.

Kamishna wa Uchumi wa Ulaya Paolo Gentiloni amebaini kwamba Umoja wa Ulaya "umejiandaa vyema" katika tukio la kusimamishwa kabisa kwa usambazaji wa gesi ya Urusi, kutokana na hatua za kuhifadhi na kuokoa nishati. "Tumejitayarisha vyema kujizatiti dhidi ya matumizi makubwa ya silaha ya gesi ambayo Urusi inatumia kama fimbo kwetu," amewaambia waandishi wa habari kando ya kongamano la kiuchumi linalofanyika nchini Italia.

Kampuni kubwa ya Gesi ya Urusi ya Gazprom ilitangaza siku ya Ijumaa kwamba bomba la gesi la Nord Stream, linalounganisha Urusi na kaskazini mwa Ujerumani, ambalo lilipaswa kuanza tena Jumamosi hii baada ya kusitishwa kwa siku tatu kwa shughuli za matengenezo, hatimaye "litasimamishwa" kabisa hadi ukarabati wa mtambo, bila kutaja tarehe ya mwisho. Kwa hivyo Moscow ilikuwa ikijibu uamuzi uliotangazwa Ijumaa na nchi za G7 kulenga nishati ya upepo ya Urusi kwa kukubali kupunguza bei ya mafuta yake.

Katika Umoja wa Ulaya, "uhifadhi wa gesi kwa sasa uko karibu 80%, kutokana na usambazaji kutoka maeneo mbalimbali", hata kama hali inatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine, alisema Bw. Gentiloni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.