Pata taarifa kuu

Wasiwasi kuhusu afya ya Elizabeth II: Familia ya kifalme yamuuguza malkia

Hofu kuhusu afya ya Malkia Elizabeth II imeongezeka Alhamisi, Septemba 8, baada ya Buckingham Palace kusema madaktari wake "wana wasiwasi". Wana wa mfalme Charles na William walimtembelea akiwa amelazwa kitandani katika makazi yake ya Balmoral.

Lango la Kasri ya Balmoral, askari wa kikosi cha ulinzi wakishika doria, Septemba 8, 2022.
Lango la Kasri ya Balmoral, askari wa kikosi cha ulinzi wakishika doria, Septemba 8, 2022. © Russel Cheyne / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano, Elizabeth II alilazimika kujiondoa kwenye mkutano uliokuwa umepangwa na washauri wake wakuu wa kisiasa, baada ya kuombwa kupumzika. "Kufuatia hali ilivyokuwa ikiendelea asubuhi ya leo, madaktari wa Malkia wanafanya kinachowezekana ili afya ya Mfalme iweze kurejea sawa na wamependekeza abaki chini ya usimamizi wa matibabu," Buckingham Palace imesema katika taarifa Alhamisi, Septemba 8.

Kauli isiyo ya kawaida kuhusiana na afya ya Malkia. Muda mfupi mapema, waraka ulipitishwa kwa Waziri Mkuu Liz Truss na wajumbe wa timu yake katika Bunge, wakitakiwa kuondoka.

Liz Truss ameandika ujumbe wa Twitter mara moja baadaye: "Nchi nzima itasikitishwa sana na habari zinazotoka kwenye Kasri la Buckingham wakati huu wa chakula cha mchana," aliandika, na kuongeza: "Mimi - na mtu nchini Uingereza -anamfikiria Malkia na familia yake kwa wakati huu. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.