Pata taarifa kuu
UJERUMANI

Kardinali wa Munich atangaza kujiuzulu baada ya kashfa za unyanyasaji wa kijinsia

Mmoja wa watu walio na ushawishi mkubwa katika kanisa Katoliki Kardinali wa Ujerumani Reinhard Marx, leo Ijumaa amemwomba Papa amvue majukumu yake kama Askofu Mkuu wa Munich, akisema anapaswa kuhusika katika jukumu la "janga" la unyanyasaji wa kijinsia uliofanywa na mapadre katika miongo ya hivi karibuni.

Reinhard Marx, mwenye umri wa miaka 67, alikuwa mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Ujerumani na rais wa Baraza la maaskofu nchini humo hadi mwaka jana, alipokataa kuwania muhula wa pili.
Reinhard Marx, mwenye umri wa miaka 67, alikuwa mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Ujerumani na rais wa Baraza la maaskofu nchini humo hadi mwaka jana, alipokataa kuwania muhula wa pili. REUTERS - Michele Tantussi
Matangazo ya kibiashara

Kujiuzulu kwake, hatua ambayo bado haijakubaliwa na Kiongozi wa kanisa Katoliki, kunakuja wakati waumini wa kanisa hilo nchini Ujerumani wamepandwa na hasira kwa unyanyasaji huo.

Wiki iliyopita, Papa Francis aliwatuma maaskofu wawili wa kigeni kuchunguza jinsi kesi za unyanyasaji wa kijinsia zilivyoshuhulikiwa na dayosisi kuu ya Cologne, ambayo ni kubwa zaidi nchini Ujerumani.

"Lazima nishusishwe katika janga la unyanyasaji wa kijinsia uliofanywa na vionozi wa Kanisa kwa miongo kadhaa iliyopita," Reinhard Marx ameandika, akiongeza kuwa alikuwa na matumaini kuondoka kwake kungeashiria mwanzo wa enzi mpya.

Reinhard Marx, mwenye umri wa miaka 67, alikuwa mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Ujerumani na rais wa Baraza la maaskofu nchini humo hadi mwaka jana, alipokataa kuwania muhula wa pili.

Tangu kuteuliwa kwake kama Askofu Mkuu mnamo mwaka 2008, mara kadhaa alitaka kukubalika zaidi kwa uhusiano wa jinsia moja na kupatikana kwa wanawake zaidi kwa majukumu ya uongozi katika kanisa linalotawaliwa na wanaume.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.