Pata taarifa kuu
LIBYA

Papa Francis ahuzunishwa na kutoweka kwa watu 130 katika Bahari ya Mediterania

Kiopngozi wa kanisa Katiliki duniani c ameeleza kuwa ni "aibu" kwa hatima ya wahamiaji 130 waliotoweka tangu siku ya Alhamisi kufuatia ajali ya meli katika Bahari ya Mediterania, na ameongeza "amesikitishwa sana na tukio hilo".

Shirika lisilo la kiserikali SOS Méditerranée lilikuwa limebaini kwamba liliona miili kadhaa kutoka pwani ya Libya karibu na boti iliyo fanya ajali na kuuwa watu 130.
Shirika lisilo la kiserikali SOS Méditerranée lilikuwa limebaini kwamba liliona miili kadhaa kutoka pwani ya Libya karibu na boti iliyo fanya ajali na kuuwa watu 130. Via REUTERS - FLAVIO GASPERINI/SOS MEDITERRANE
Matangazo ya kibiashara

“Ninaaambia kwamba nimehuzunishwa sana na mkasa huo ambao ulitokea tena kwa siku za hivi karibuni katika Bahari ya Mediterania. Ndugu na dada, hebu sote tujiulize juu ya janga hili la kumi na moja. Ni wakati wa kila mtu kuona aibu, ”Papa Francis amewaambia waamini baada ya sala ya Regina Coeli, katika eneo la Mtakatifu Peter huko Vatican.

Walikuwa na "siku mbili kamili wakiomba msaada " “Wahamiaji mia na thelathini walifariki dunia wakiwa baharini, hawa ni watu, haya ni maisha ya wanadamu ambao kwa siku mbili nzima waliomba msaada bila kujibiwa. Msaada ambao haujafika, ”amebaini Papa Francis. “Tuwaombee hawa kaka na dada na kwa wengine wengi ambao wanaendelea kufariki dunia katika safari hizi kubwa. Tuwaombee pia wale ambao wanaweza kusaidia lakini wanaamua kupuuzia. Wacha tuwaombee kimya kimya, ”amesema Papa.

Shirika lisilo la kiserikali SOS Méditerranée lilikuwa limebaini siku ya Alhamisi, Aprili 22 kuwa liiliona miili kadhaa kutoka Libya karibu na boti iliyopinduka ambayo ilikuwa imeripotiwa kuwa na tatizo na likiwa na watu wapatao 130.

Umoja wa Ulaya wanyooshewa kidole

Mashirika yakutoa misaada yanashutumu nchi za Umoja wa Ulaya sio tu kwamba hawataki kuwaokoa wahamiaji walio katika hatari katika Bahari ya Mediterania, lakini pia kwa kukwamisha shughuli zao za uokoaji.

Kulingana na takwimu kutoka Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) wahamiaji wasiopungua 453 wamekufa tangu Januari 1, 2021 katika Bahari ya Mediterania, hasa katika njia hii kuu kutoka Tunisia na Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.