Pata taarifa kuu

Papa Francis aomba kulindwa kwa Wakiristo nchini Iraq

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, amekutana na kiongozi wa  Kiislamu wa dhehebu la Kishia Ayatollah Ali al-Sistani, mjini Najaf nchini Iraq na kutoa wito wa amani, huku akiwataka Waislamu kuishi kwa amani na Wakiristo walio wachache nchini humo.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis (Kulia) akiwa na kiongozi wa Kiislamu wa Kishia Ayatollah Ali al-Sistani mjini Najaf, nchini Iraq, Jumamosi, Machi 6, 2021, katika ziara ya kwanza ya kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini humo.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis (Kulia) akiwa na kiongozi wa Kiislamu wa Kishia Ayatollah Ali al-Sistani mjini Najaf, nchini Iraq, Jumamosi, Machi 6, 2021, katika ziara ya kwanza ya kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini humo. AP
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu wa kihistoria umefanyika siku ya Jumamosi katika makaazi ya al Sistani, mkutano ambao hatimaye umefanyika baada ya miezi kadhaa ya maandalizi kabla ya viongozi hao kukutana.

Baada ya kiko hicho, Ofisi ya kiongozi huyo wa Kiislamu amesema dini na viongozi wake, wanawajibu wa kuwalinda Wakiristo walio wachache nchini Iraq, na kuwahakikishia kuwa , wataishi kama raia wengine nchini humo na kufurahia haki zao.

Papa Francis amemshukuru Ayatollah al Sistani kwa kuwa katika mstari wa mbele, kupaza sauti kuwatetea Wakiristo wachache dhidi ya dhuluma ambazo wamekuwa wakipîtia katika miaka kadhaa sasa.

Papa Francis anazuru Iraq, licha ya kuwepo kwa janga la Corona na tishio la usalama nchini humo na anakuwa kiongozi wa kwanza wa Kanisa hilo kuwahi kutembelea nchi hiyo ya Kiislamu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.