Pata taarifa kuu
UINGEREZA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Uingereza, nchi ya tano kwa zaidi ya vifo 15,000

Mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 umesababisha vifo vya watu zaidi ya 888 katika masaa 24 katika hospitali mbalimbali nchini Uingereza, na kusababisha jumla ya vifo 15,464, Waziri wa Afya amesema jana Jumamosi.

Malkia Elisabeth II na Prince Philip, wakati waziara yao Kusini mwa Uingereza, Juni 4, 2016.
Malkia Elisabeth II na Prince Philip, wakati waziara yao Kusini mwa Uingereza, Juni 4, 2016. GLYN KIRK / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kati ya vipimo 357,023 vilivyofanywa, watu 114,217 wamepâtikana waliambukizwa virusi vya Coronai, Waziri wa Afya amesema.

Watu 980 walifariki dunia Aprili 9, ikiwa ni idadi kubwa kabisa katika ripoti inayotolewa kila siku nchini Uingereza. Kwa wiki nzima idadi iliyo chini ya vifo vya watu 800 iliripotiwa lakini idadi hiyo ilianza kuwa juu tangu Jumatano.

Uingereza ni nchi ya tano iliyoathiriwa zaidi katika suala la vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa COVID-19, baada ya Marekani, Italia, Uhispania na Ufaransa.

Kutokana na ugonjwa huo, Malkia Elizabeth II ameomba zoezi la kijadi la kufyatua mizinga hewani kwa sherehe ya kuzaliwa kwake lifutwe, televisheni ya ITV News imeripoti, ikiwa ni mara ya kwanza katika miaka sitini na nane ya utawala wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.