Pata taarifa kuu
UINGEREZA-JOHNSON-CORONA-AFYA

Boris Johnson awashukuru watalaam wa afya kwa kuokoa maisha yake

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameruhusiwa kuondoka hospitali, baada ya kupata nafuu kutokana na mamabukizi ya Corona, ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya Elfu 10.

Wazir Mkuu wa Uingereza Boris Johnson.
Wazir Mkuu wa Uingereza Boris Johnson. REUTERS/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Ongezeko hili la vifo limezua huzuni nchini humo, huku Waziri Mkuu Johnson akiwashukuru watalaam wa afya kwa kuokoa maisha yake.

Waziri Mkuu wa Uingereza alikiri na kuwataja kwa majina wahudumu kadhaa wa Shirika la Huduma za Afya, NHS, ambao waliyaokowa maisha yake, baadhi yao wakiwa na asili ya kigeni.

Boris Johnson, mwenye umri wa miaka 55 alilazwa tarehe 5 Aprili, ambako alikaa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku tatu mfululizo.

Boris Johnson hadi sasa ndiye kiongozi wa juu kabisa duniani kuuguwa ugonjwa wa COVID-19 kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Akilihutubia taifa kwa njia ya vidio, Waziri Mkuu wa Uingereza alielezea imani yake kwamba Uingereza itautokomeza ugonjwa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.