Pata taarifa kuu
UINGEREZA-CORONA-AFYA

Waziri Mkuu Boris Johnson apatikana na virusi vya Covid-19

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amepatikana na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19, baada ya kufanyiwa vipimo na kuonyesha "dalili ndogo za virusi hivyo Alhamisi wiki hii," ofisi ya waziri mkuu (Downing Street) imebaini leo Ijumaa.

Boris Johnson katika mkutano na waandishi wa habari huko London, Machi 20, 2020.
Boris Johnson katika mkutano na waandishi wa habari huko London, Machi 20, 2020. Julian Simmonds/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Baada ya kuonekana kwa dalili ndogo za virusi vya Corona Alhamisi wiki hii, Waziri Mkuu amepimwa ugonjwa wa Covid-19" na "matokeo ni kwamba amepatikana na virusi vya ugonjwa huo," msemaji wa ofisi ya waziri mkuu amesema katika taarifa.

Katika video iliyorushwa hewani kwenye Twitter, Boris Johnson mwenye umri wa miaka 55 ameeleza kwamba alikuwa "amejiweka mwenyewe karantini", huku akibaini kwamba aliendelea "kuetekeleza majukumu yake ya waziri mkuu na kuendesha mikutano mbalimbali ya serikali kupitia video.

"Nilionyesha dalili ndogo za Coronavirus na nilipimwa na nikakutwa na ugonjwa wa Covid-19. Kwa hivyo, ninafanya kazi nikiwa nyumbani, nilijiweka mwenyewe karantini. Na hivyo ndivyo watu wanatakiwa kufanya iwapo wanajihisi kuwa wameambukizwa virusi vya Corona. Lakini msiwe na hofu kuwa nitaendelea kuwasiliana na timu yangu yote ili kujibu majibu ya serikali kupitia video wakati huu tunapambana na virusi hivi. Nataka kuwashukuru wale wote wanaohusika na hasa, timu zetu katika mfumo mzima wa afya katika ngazi ya kitaifa. Napenda kuwashukuru wale wote ambao wanapelekea nchi yetu iendelea kujidhatiti kimaisha licha ya janga hili. Asante pia kwa wote wanaofuata mfano wangu: waendelee kufanya kazi nyumbani ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona. Hivi ndivyo tutashinda. Kaeni nyumbani, linda mfumo wa afya na muokoe maisha ya watu. "

Mkewe Carrie Symonds, ambaye ni mjamzito, tayari yuko karantini, kufuata maagizo ya serikali. Tangazo hili linakuja baada ya mwanamfalme Charles, 71, kupatikana na virusi vya Corona na "bado yuko katika afya njema" kwa mujibu wa wasaidizi wake.

Wajumbe wa baraza lake la mawaziri, pamoja na washauri wake wakuu wa matibabu na kisayansi na wabunge wengi, wanatarajiwa kupimwa na kuamua kujitenga wenyewe. Ikiwa afya ya kiongozi huyo wa Uingereza itadhoofika, Dominic Raab, Waziri wa Mambo ya nje anatarajiwa kuchukua madaraka, kulingana na ripoti ya mwandishi wetu huko London, Muriel Delcroix.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.