Pata taarifa kuu
UFARANSA-SANGARIS

Uchunguzi kuhusu askari wa Sangaris CAR kuanza

Mahakama ya Ufaransa imeanzisha uchunguzi unaolenga askari wa kikosi cha Sangaris, wanaotuhumiwa kuwapiga raia wawili kutoka Jamuhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2014 katika mji wa Bangui, nchini Jamhuri ya Afrika (CAR), au "kufumbia macho vitendo viovu".

Askari kumi na nne wa Ufaransa walioko kwenye operesheni Sangaris wanatuhumiwa katika kesi za unyanyasaji wa kijinsia, lakini wachache wametambuliwa.
Askari kumi na nne wa Ufaransa walioko kwenye operesheni Sangaris wanatuhumiwa katika kesi za unyanyasaji wa kijinsia, lakini wachache wametambuliwa. AFP PHOTO / MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya mashitaka ya mjini Paris imeanzisha uchunguzi wa mwanzo, hasa kwa "machafuko yaliyoendeshwa kimakusudi katika mkutano", "vitisho kwa kutumia silaha" na "kutojali watu walio katika matatizo." Kesi mya ambayo inalikabili jeshi la Ufaransa baada ya kashfa ya hivi karibuni kuhusu unyanyasaji wa kingono.

Askari kutoka kambi ya kikosi cha wanamaji, walioko magharibi mwa Ufaransa, wanakabiliwa na mkono wa sheria.

Askari hao wanatuhumiwa kutekeleza au kufumbia macho vitendo viovuvilivyofanyiwa raia wawili wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati katika kituo cha ukaguzi cha mtaa wa PK 12, mjini Bangui. Tukio hili lilitokea katika wiki ya kwanza ya mwaka 2014.

Mwanzoni mwa mwezi Juni, "kutokana na uzito wa vitendo hivyoi," Wizara ya Ulinzi "ilichukua hatua ya kuwasimamisha kazi" askari watano. Wengine wanne pia waliadhibiwa, kwa sababu "walishuhudia tukio hilo, hawakutoa ripoti," Wizara ya Ulinzi ilisema katika taarifa yake.

Kesi hii ya kuwapia raia hao wawili "haiendani na unyanyasaji wa kingono," amesema afisa wa Wizara ya Ulinzi aliyenukuliwa na OUEST-FRANCE, gazeti lililoweka wazi tukio hilo.

Itafahamika kwamba kikosi cha askari wa Ufaransa cha Sangaris tayari kuhusishwa na kashfa ya madai ya unyanyasaji au udhalilishaji wa kingono, sawa na askari wa kulinda amani, askari wengine wa kigeniwaliokua wakisimamia amani na usalama nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati. Kutokana na hali hiyo, faili tatu za uchunguzi zimeanzishwa na mahakama ya jijini Paris. Askari watano walisikilizwa kufuatia tuhuma hizo, lakini hadi sasa hakuna aliyefunguliwa mashitaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.