Pata taarifa kuu
UFARANSA-JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Usalama

CAR: mwanahabari wa Ufaransa auawa

Mwandishi wa habari na mpiga picha mwenye asili ya Ufaransa Camille Lepage mwenye umri wa miaka 26 ambaye ameuawa katika hali ambayo ni ya kutatanisha wakati akiandaa ripoti nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Muandishi wa habari akiwa pia mpiga picha, raia wa Ufaransa Camille Lepage, hapa ilikua Februari mwaka 2014 wakati alipokua katika kazi yake ya kutafuta habari, mjini Bangui. à Bangui.
Muandishi wa habari akiwa pia mpiga picha, raia wa Ufaransa Camille Lepage, hapa ilikua Februari mwaka 2014 wakati alipokua katika kazi yake ya kutafuta habari, mjini Bangui. à Bangui. AFP PHOTO / FRED DUFOUR
Matangazo ya kibiashara

Mwili wa Camille Lepage umepatiakana kwa msaada wa vikosi vya Ufaransa vya operesheni Sangaris ambavyo vimekua vikipiga doria na ukaguzi wa gari moja iliyokuwa inaendeshwa na wanamgambo wa Anti-Balaka katika eneo la Bouar (magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati) kwenye mpaka na nchi jirani ya Cameroon na ya Chad.

Serikali ya Ufaransa kwa upande wake imeahidi kuendesha uchunguzi ili kubaini mazingira ya mauwaji hayo na kuendelea kutoa mchango wake kwa ajili ya amani nchini humo

Kwa mujibu wa mmoja wa wawaanzilishi wa shirika la habari Hans Lukas, amabalo ilimuajiri mwandishi huyo wa habari, Camille Lepage, alikua anaipenda kazi yake ya uandishi wa habari, na hakua na uoga wa kitu chochote ambacho kinaweza kumtokea.

Kwa mujibu wa mama yake mzazi, Camille Lepage amekua akijaribu kuwafikia watu waliosahaulika, na ambao maisha yao yamo hatarini. Hali hio ndio iliompelekea mwandishi huyo wa habari kujielekeza nchini Sudani Kusini, na baadae Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mwandishi wa habari mwenye asili ya Ufaransa, Camille Lepage akiwa mjini Damara (CAR), kilomita 70 kaskazini mwa mji wa Bangui, Februari 21 mwaka 2014.
Mwandishi wa habari mwenye asili ya Ufaransa, Camille Lepage akiwa mjini Damara (CAR), kilomita 70 kaskazini mwa mji wa Bangui, Februari 21 mwaka 2014. AFP / FRED DUFOUR

Muili wa Camille Lepage umesafirishwa katika mji wa Bouar ili usafirishwe kwa ndege katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui.

Serikali ya Ufaransa kwa upande wake imeahidi kuendesha uchunguzi ili kubaini mazingira ya mauwaji hayo na kuendelea kutoa mchango wake kwa ajili ya amani nchini humo.

Hii ni moja ya picha alizopiga Camille Lepage nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mwanamgambo wa kundi la kikristo la anti-balaka, ambayr ni mkaazi wa mji wa Bossembele kaskazini magharibi mwa mji wa Bangui, Februari 24 mwaka 2014. 2014.
Mwanamgambo wa kundi la kikristo la anti-balaka, ambayr ni mkaazi wa mji wa Bossembele kaskazini magharibi mwa mji wa Bangui, Februari 24 mwaka 2014. 2014. REUTERS/Camille Lepage

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.