Pata taarifa kuu
CAR-UFARANSA-SANGARIS-USALAMA

Mwaka mmoja baada ya vurugu kutokea CAR

Desemba 5mwaka 2013, Ufaransa ikiwa chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa, ilianzisha operesheni ya kijeshi iliyoiita Sangaris nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Askari wa kikosi cha Ufaransa Sangaris wakipiga doria pembezoni mwa mji wa Boda, kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya kati, Julai 24 mwaka 2014.
Askari wa kikosi cha Ufaransa Sangaris wakipiga doria pembezoni mwa mji wa Boda, kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya kati, Julai 24 mwaka 2014. AFP PHOTO / ANDONI LUBAKI
Matangazo ya kibiashara

Lengo ilikua kukomesha machafuko yaliyotokea kati ya wenyewe kwa wenyewe, baada ya aliye kuwa rais wa nchi hiyo Francois Bozize kutimuliwa madarakani na waasi wa Seleka mwaka 2012. Askari 2,000 wa Ufaransa waliingilia kati ili kusaidia askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika Misca na baadae kikosi cha Umoja wa Mataifa katika majukumu yao ya kulinda usalama wa nchi na kuwalinda raia.

Majeshi ya Ufaransa yalipoteza askari watatu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Lakini kikosi hicho cha wanajeshi wa Ufaransa kilipata mafanikio makubwa katika operesheni hiyo, na vilevile kililaumia kutowalindia usalama baadhi ya raia, hususan jamii ya Waislam katika mji Bangui.

Mwaka mmoja baadaye, hali imekuwa nzuri kiasi fulani katika sekta ya usalama, lakini lengo la kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati halijakamilika.

Hata hivyo hali ya usalama bado ni tete katika baadhi ya maeneo ya mji wa Bangui. Mwanzoni mwa mwezi Oktoba, watu 11 waliuawa na wengine 200 walijeruhiwa katika machafuko yaliyotokea baada ya mtu mmoja kurusha gruneti sokoni.

Kwa leo, kikosi cha Umoja wa Mataifa ndio kinahusika na kusimamia usalama. Idadi ya askari wa Ufaransa wamepunguzwa katika mji wa Bangui, lakini wametumwa katika mikoa ili kufungua barabara inayotumiwa kwa kuingiza chakula katika mji wa Bangui kikitokea cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.