Pata taarifa kuu
UFARANSA-CAR-UBAKAJI-SHERIA

Askari wa Ufaransa wasikilizwa kuhusu tuhuma za ubakaji CAR

Kesi kuhusu ubakaji unaoshukiwa kutendwa na wanajeshi wa Ufaransa iliwekwa wazi katika majira ya joto mwaka 2015 na gazeti la kila siku la Uingereza The Guardian.

Askari wa Ufaransa wa kikosi cha opereshini Sangaris wakipiga doria katika mji wa Bria, Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Aprili 2014.
Askari wa Ufaransa wa kikosi cha opereshini Sangaris wakipiga doria katika mji wa Bria, Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Aprili 2014. © AFP PHOTO / MIGUEL MEDINA
Matangazo ya kibiashara

Watoto wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaoishi katika kambi ya M'Poko jijini Bangui wanasema walinajisiwa na askari wa Ufaransa wa kikosi kinachosimamia amani Afrika ya kati (Sangaris).

Shutma hizo zimesababisha kuanzishwa kwa uchunguzi wa mahakama nchini Ufaransa, na hii Jumanne, Desemba 8, askari wanne wamesikilizwa na polisi maarufu kwa uchunguzi.

Askari wanne kutoka kambi ya 152 ya wanajeshi wa nchi kavu ya Colmar, mashariki mwa Ufaransa, wamesikilizwa. Moja yuko chini ya ulinzi, watatu wengine watatu wamesikilizwa wakiwa huru na polisi mashuhuri kwa uchunguzi, huku wakipewa mwanasheria wa kuwasadia.

Kitengo hiki cha polisi ya taifa kinahusika na uchunguzi wa makosa yaliyofanywa na wanajeshi wa Ufaransa waliotumwa katika operesheni mbalimbali za kijeshi nje ya nchi.

Kitengo hiki cha polisi kiliwahi kuwatuma mara mbili wachunguzi jijini Bangui, ambao waliwahoji watoto kumi na mmoja, wanaoshukiwa kutendewa ubakaji. Kitengo hiki cha polisi pia kinatarajiwa katika siku zijazo kusikia muhusika wa ripoti ya Umoja wa Mataifa ilioelezea uwezekano wa makosa haya. Hata hivyo ili afisa huyu wa Umoja wa Mataifa asikilizwe inabidi aondolewe kinga yake ya kisheria.

Wachunguzi pia wana uchunguzi wa ndani uliofanywa na jeshi wakati lilipata taarifa kuhusu mkasa huo wa kuwanajisi watoto, miezi tisa kabla ya uchapishaji wa makala katika gazeti la The Guardian. Nyaraka hizi zilitolewa kwa ombi la Ofisi ya mashitaka ya jiji la Paris. Wizara ya Ulinzi, ambayo ilikosolewa kwa kukosa kuwasiliana ilipopata taarifa hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.