Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Urusi yadai kucukuwa udhibiti wa kijiji kipya magharibi mwa Avdiïvka

Urusi imedai leo Alhamisi, Machi 21, kuchukuwa udhibiti wa kijiji cha Tonenke, kilichoko magharibi mwa mji wa Avdiïvka kilichochukuliwa mwezi Februari, ikiendelea na mwendo wake wa polepole dhidi ya jeshi la Ukraine linalokabiliwa na ukosefu wa wanajeshi na risasi.

Askari wa Ukraini akiwa amebeba ndege isiyo na rubani karibu na mji wa Avdiivka katika jimbo la Donetsk, karibu na eneo la mapigano, Februari 17, 2023.
Askari wa Ukraini akiwa amebeba ndege isiyo na rubani karibu na mji wa Avdiivka katika jimbo la Donetsk, karibu na eneo la mapigano, Februari 17, 2023. AP - LIBKOS
Matangazo ya kibiashara

"Katika eneo la Avdiïvka, kijiji cha Tonenke (...) lilikombolewa kutokana na hatua zilizoratibiwa za vitengo vya kikundi cha askari kutoka eneo la Kati," Wizara ya Ulinzi imesema katika ripoti yake ya kila siku.

Mashambulio ya Urusi kwenye vijiji kadhaa

Kulingana na kituo cha Telegram cha Rybar, kilicho na ukaribu na jeshi la Urusi na kikifuatiwa na zaidi ya watu milioni 1.2, vikosi vya Moscow vinajaribu katika sekta hii kufikia ukingo wa kushoto wa mto wa eneo hilo ili kuzindua mashambulizi kuelekea vijiji vya Semenivka na Oumanské.

Vikosi vya Urusi vimekuwa vikishika kasi mbele tangu kutekwa kwa mji wa Avdiïvka katikati ya mwezi wa Februari, ambao ulikuwa kama ngome ya jeshi la Ukraine.

Ikichoshwa na uvamizi wake ulioshindwa katika msimu wa joto wa mwaka 2023 na kukabiliwa na ukosefu wa risasi kwa sababu ya kucheleweshwa kwa msaada wa nchi za Magharibi, Ukraine ilianza haraka baada ya kupoteza mji wa Avdiïvka, kujenga safu za ulinzi ili kusimamisha operesheni za Urusi.

Mashambulizi makubwa dhidi ya Kyiv

Urusi pia imefanya shambulio la kwanza kubwa la kombora katika mji mkuu wa Kyiv tangu kuanza kwa uvamizi wake nchini Ukraine mwezi wa Februari, alfajiri siku ya Alhamisi, baada ya kuapa kulipiza kisasi kwa mashambulizi mabaya ya hivi karibuni ya Ukraine katika maeneo ya mpaka wa Urusi.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imehakikisha kwamba ilishambulia"vituo vya maamuzi, kambi za vifaa vya kijeshi na maeneo mengine ya kijeshi" ya vikosi vya Ukraine na "imaeneo yote hayo yamelengwa". Ukraine, kwa upande wake, imedai kudondosha makombora yote 31 yaliyorushwa na Moscow.

Jeshi la Urusi pia limebaini kwamba "linachukua hatua za kuzuia kupenya kwa makundi ya upelelezi ya vikosi vya Ukraine" katika eneo la Belgorod, lengo tangu wiki iliyopita la uvamizi wa silaha na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.