Pata taarifa kuu

Vikosi vya kijeshi vya Ukraine vinashikilia shinikizo kwa Crimea

Miaka kumi baada ya kunyakuliwa kwake na Urusi, Crimea inayokaliwa leo ni moja ya malengo ya kipaumbele ya vikosi vya jeshi la Ukraine. Kyiv inaongeza juhudi zake na kufanya operesheni za kijeshi za ujasiri kujaribu kuteka tena rasi hiyo.

Maelezo ya video ya uchunguzi inayoonyesha moshi juu ya makao makuu ya jeshi la wanamaji la Urusi huko Sevastopol, Crimea, mnamo Septemba 22, 2023, baada ya shambulio la Ukraine.
Maelezo ya video ya uchunguzi inayoonyesha moshi juu ya makao makuu ya jeshi la wanamaji la Urusi huko Sevastopol, Crimea, mnamo Septemba 22, 2023, baada ya shambulio la Ukraine. © Canal criméen sur Telegram / via AP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za anga na baharini, mashambulizi ya ardhini, vikosi vya jeshi vya Ukraine vinadumisha shinikizo katika jimbo la Crimea, ambalo ni eneo muhimu la usafirishaji wa wanajeshi wa Urusi. Kutenga Crimea ili kupunguza usambazaji wa wanajeshi na vifaa "ni muhimu sana kwetu, kwa sababu ndio njia ya kupunguza idadi ya mashambulio kutoka jimbo hili", alisema Volodymyr Zelensky mwanzoni mwa mwaka katika mahojiano na Gazeti la The Economist , akisisitiza kwamba "Crimea na vita katika Bahari Nyeusi (vitakuwa) kitovu cha ukubwa wa vita".

"Mshangao" mpya unakuja Crimea

Mapema mwezi huu, idara ya ujasusi ya kijeshi ya Ukraine ilitoa video ya madai ya shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye boti ya kisasa ya doria ya Urusi, Sergei Kotov. Mwisho wa mwezi Desemba, moja ya meli kubwa zaidi za kivita za amphibious, Novocherkassk, ilipigwa na makombora ya masafa marefu katika bandari ya Feodosiya. Miezi mitatu kabla ya hapo, wanajeshi wa Ukraine walishambulia kwa mabomu makao makuu ya jeshi la majini kwenye Bahari Nyeusi huko Sevastopol.

Mkuu wa ujasusi wa kijeshi wa Ukraine Kyrylo Budanov ametangaza kwamba "mshangao" mpya unaokuja kwenye rasi ya Crimera, akisisitiza kwamba vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vilianza sio miaka miwili iliyopita, lakini miaka kumi iliyopita, na kukaliwa kwa Crimea, moja ya majimbo ya Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.